Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shukrani sana mkuu. Moyo wa uvumilivu ndani una amani
 
Emoj naiba za kwenu mnazoweka hapa life inaendelea maisha bila emoj inawezekana. Pia notification nazipata nikiingia humu basi. Nisipoingia sizipati na ndo nachopenda sio kila saa mlio wa sms kama watsup
 
Gmorning too
 
Kwa hakika kila jambo lenye uzuri au faida lina hasara zake. Nafahamu umekuwa ukisikia faida kede kede za kusikiliza mziki, lakini haujasikia kuwa kwa upande mwingine mziki unaweza kuwa na madhara kwako.
 
Huathiri afya ya masikio

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kumeibuka vifaa mbalimbali katika swala la utengenezaji, usambazaji na hata usikilizaji wa mziki.

Kutokea kwa teknolojia ya vifaa vya kusikilizia mziki vijulikanavyo kama headphones au earphones kumesababisha watu wengi hasa vijana kusikiliza mziki karibu kila mahali na kila wakati.
 
Taarifa mbalimbali za kitabibu zinaeleza kuwa vifaa hivi vimechangia sana kuharibu masikio au mfumo wa kusikia wa watumiaji wengi wa vifaa hivi; kwani wengi huvivaa siku nzima au usiku kucha.

Hivyo kusikiliza mziki sana hasa kwa kutumia headphones au earphones kunaweza kuathiri afya ya masikio yako, hivyo ni vyema kuwa na kiasi.
 
Huchangia kuharibu maadili

Miziki ya leo hasa ile inayofahamika kama miziki ya kizazi kipya, hujumuisha maudhui mengi ambayo ni kinyume cha maadili.

Katika miziki hii wasanii hutumia lugha chafu, huvaa mavazi ya aibu, au hata kufanya matendo ya aibu katika miziki iliyowekwa kwenye video.
 
Hili limesababisha watoto na vijana wengi kuiga tabia hizi ambazo kimsingi ni kinyume cha maadili mema. Hivyo kusikiliza au kutazama miziki hii kunaweza kuathiri maadili yako kama hutokuwa na utawala mzuri wa kifikra na kimaamuzi.
 
Huvuruga utendaji kazi

Kuna watu wanaosikiliza mziki kwa kiwango cha kupitiliza; watu hawa husikiliza mziki kazini, nyumbani, au hata darasani.

Swala hili linaweza kuathiri ufanisi wako kwani mara nyingi mziki utachangia kukusababisha usijikite kwenye kile unachopaswa kufanya.

Hebu fikiri mtu yuko darasani anamsikiliza mwalimu huku akiwa amevaa headphones au earphones; je ataweza kuelewa kweli kinachofundishwa? Ni wazi kuwa hatoweza kuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…