Nauza maziwa lita moja kwa Sh1,500, ni kiasi kidogo kwangu kwa sababu wateja wa maziwa siyo wengi. Naamini kama soko lingekuwa zuri, ningepata zaidi ya Sh 1milioni kwa mwezi.’’
Mmakuwa hakuwahi kuajiriwa, lakini kupitia ufugaji wa ng’ombe amejenga nyumba nzuri huku akijinasibu kuwa nyumba hiyo haina tofauti na nyinginezo zinazomilikiwa na watu wenye ajira. Kikubwa ni malengo, wazo la kujenga lilikuja baada ya kufikisha ng’ombe watano. Niliuza watatu nikanunua kiwanja, nikasuburi tena kila wakiongezeka nauza, nilijenga taratibu kwa muda wa miaka sita hadi kukamilisha ujenzi kupitia mifugo yangu.’’