Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Robaldo yafaa amuige Zidane
 
Miezi 30 baadaye ameamua kutuacha tena vile vile. Zizzou ametangaza kubwaga manyanga pale Real Madrid. Nani alitegemea hili litatokea? Sidhani kama yupo.

Zizzou ametangaza kuachana na Madrid siku sita tu, baada ya kuipa Real Madrid taji la tatu la UEFA, tena mfululizo. Anaondoka wakati kwenye miaka yake miwili na nusu klabuni hapo ameshinda mataji sita likiwamo moja la La Liga ambalo Madrid walikuwa wanalisotea kwa miaka mitano.
 
Anaondoka wakati dunia inamtazama kama Kocha Bora kwa ngazi ya klabu kwa sasa. Mafanikio yake yalitosha kumbakiza pale Real Madrid kwa miaka mingi zaidi. Hata hivyo ameondoka kimaajabu vilevile.

Maajabu ya Zizzou hayajawahi kutuacha salama hata kidogo. Maajabu mengine yanaweza kutokea kwa timu anayotaka kwenda kwa sasa.
 
Wakati wadau wengi wa soka wakijiuliza kuwa Zizzou anakwenda kufundisha klabu gani nyingine kubwa duniani, tetesi zimeanza kumhusisha na timu ya taifa ya Qatar. Inastaajabisha sana.

Zizzou kwa sasa si mtu wa kwenda kuhangaika na timu za taifa. Tena zaidi si mtu wa kwenda kuhangaika na taifa dogo kama Qatar ambayo haiwezi kushinda taji lolote kubwa duniani.
 
Licha ya kwamba Qatar inaandaa michuano ijayo ya Kombe la Dunia, bado ni timu ndogo sana kwa Zizzou. Tungemwelewa Zizzou kama angechukua timu ya Taifa ya Ufaransa ama taifa jingine kubwa lakini sio Qatar.

Pia baada ya mataji matatu ya UEFA na Madrid, tulitarajia Zizzou atakwenda kwenye Ligi ya Ujerumani, Ufaransa ama England ili kuendelea kuthibitisha ubora wake zaidi. Ni kama vile Pep Guardiola alivyoondoka Barcelona mwaka 2012.
 
Lakini kwa namna Zizzou alivyo na akili yake, ni ngumu kufanya kile tunachokifikiria. Zizzou anaamini katika kile ambacho akili yake inamwambia. Kama aliweza kumpiga kichwa Materazzi kwenye fainali ya Kombe la Dunia, anashindwaje kwenda Qatar? Binafsi ningependa zaidi kumuona Zizzou akiendelea kufundisha soka la klabu.
Robaldo yafaa amuige Zidane
.
Wivu tu
 
Lakini kwa namna Zizzou alivyo na akili yake, ni ngumu kufanya kile tunachokifikiria. Zizzou anaamini katika kile ambacho akili yake inamwambia. Kama aliweza kumpiga kichwa Materazzi kwenye fainali ya Kombe la Dunia, anashindwaje kwenda Qatar? Binafsi ningependa zaidi kumuona Zizzou akiendelea kufundisha soka la klabu.
 
Numby una bias kwa Ronaldo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…