Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kama dili hilo likigoma kukamilika kuna uwezekano mkubwa Ronaldo akaachana na Real Madrid mwaka huu huku Manchester United na PSG zikitajwa huenda zikavamia kwenda kumnyakua Mreno huyo ambaye hatima yake itafahamika wazi baada ya fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Russia baadaye mwezi huu.
 
Tatizo jingine litakalomkimbiza Ronaldo kutoka Madrid ni mamlaka ya kodi ya Hispania ambayo inaonekana kumbana mchezaji huyo huku akitaka timu yake imlinde kwa mambo kama hayo.
 
Ripoti zinadai kwamba Mourinho hawezi kupokea ofa yoyote ya kumuuza kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa. Anachosema Mreno huyo ni kwamba Pogba yupo kwenye mipango yake akiamini msimu ujao atakuwa matata zaidi atakapocheza kwenye safu ya viungo watatu sambamba na Nemanja Matic na Mbrazili Fred.
 
Real Madrid, Barcelona na Juventus zimeripotiwa kufukuzia huduma ya Pogba katika dirisha hili la usajili.

Pogba wiki iliyopita alizungumzia uhusiano wake na Mourinho ambapo alisema: “Yeye (Mourinho) aliniweka kwenye benchi, nilimjibu uwanjani na nilijitolea kwa uwezo wangu muda wote. Kuna kipindi ambacho sikucheza, nikiwa benchi, watu walizungumza mengi sana. Watu walidhani hilo ni tatizo, lakini siku zote kocha na mchezaji hawawezi kuwa marafiki wakubwa.”
 
USIKU mmoja tulivu katikati ya mwaka 2006. Usiku wa siku muhimu ya fainali ya Kombe la Dunia. Usiku wa fainali.

Kazi kubwa ilikuwa imefanyika na hadi kufikia usiku huo, nahodha wa Ufaransa, Zinedine Zidane ‘Zizzou’ ndiye alikuwa staa mkubwa. Akielekea ukingoni mwa maisha yake ya soka, Zizzou alikuwa ameibeba Ufaransa mabegani mwake.
 
Alikuwa akirudia kile alichokifanya kwenye fainali za mwaka 1998. Alionyesha kiwango bora katika michuano hiyo. Aliipeleka Ufaransa fainali hizo zilizofanyika katika nchi ya Ujerumani kwa uwezo wake binafsi. Ufaransa haikuwa na maajabu makubwa zaidi ya uwepo wa Zizzou.
 
Alikuwa ndiye nahodha wa timu. Ufaransa nzima ilimtazama Zizzou. Dunia nzima ilimtazama Zizzou. Alikuwa amewavuruga akina Ronaldinho Gaucho na Brazil yao kwenye pambano la robo fainali. Alikuwa kwenye ubora wa juu.
 
Pamoja na yote, usiku huo wa fainali Zizzou hakutuacha salama. Wakati Ufaransa yote ikimtazama Zizzou kama mkombozi wao. Wakati Dunia ikimtazama Zizzou kama mtu anayekwenda kuipa taji timu hiyo, alituacha kimaajabu.
 
Zizzou anaifahamu akili yake mwenyewe. Anajijua mwenyewe. Huwa anafanya mambo kwa namna akili yake inavyomwongoza na si dunia ya nje inamtazamaje.

Mechi dhidi ya Italia ilikuwa imenoga. Mpaka dakika 15 za muda wa ziada zinaelekea kumalizika matokeo yalikuwa bao 1-1. Zizzou alitarajiwa kufanya maajabu yake, lakini akatuacha kimaajabu.
 
Kama dili hilo likigoma kukamilika kuna uwezekano mkubwa Ronaldo akaachana na Real Madrid mwaka huu huku Manchester United na PSG zikitajwa huenda zikavamia kwenda kumnyakua Mreno huyo ambaye hatima yake itafahamika wazi baada ya fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Russia baadaye mwezi huu.
Asje man utd aende psg
 
Wakati tukitarajia Zizzou afanye miujiza ya kuisaidia Ufaransa, yeye aliamua kutuaga kwenye soka. Alimpiga kichwa Marco Materazzi wa Italia kwenye dakika hizo za nyongeza.

Materazzi alimtukana Zidane. Inasemakana alimtolea lugha chafu za kibaguzi. Lakini kwa uzoefu wa Zidane na heshima yake kwa dunia, haikutarajiwa kama angefanya tukio lile. Zizzou hakujali sana, aligeuka kibabe na kumchapa Materazzi kichwa safi cha kifuani.
 
Mwamuzi akamwonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja. Wala hakujali sana. Akavua kitambaa cha unahodha na kutoka nje kistaarabu. Matokeo yake Ufaransa ilipoteza pambano hilo kwa mikwaju ya penalti. Inaumiza sana.

Baada ya pambano, Zizzou alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia. Pamoja na uchaguzi huo, Zizzou alitangaza kuachana na soka la ushindani. Si tu aliiacha timu ya taifa ya Ufaransa, bali aliachana na soka kabisa. Akastaafu na pale Real Madrid.
 
Ilishangaza sana. Zidane alikuwa ndio kwanza ana miaka 34. Kiwango chake bado kilikuwa cha juu. Alikuwa ndiye Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia. Nani alitarajia Zizzou angetuacha kwa namna ile? Hakuna.

Hata hivyo Zizzou huwa anafanya anachokiamini. Huwa anafanya kile ambacho anafikiri ni sahihi kwake, sio kwa wengine.
 
Ndio maana alimpiga kichwa Materazzi, akaondolewa kwenye fainali lakini akachaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Kombe la Dunia na akaamua kuachana na soka usiku huo huo. Ilishangaza sana.

Bahati nzuri, Zizzou alizaliwa upya akiwa kocha. Miaka miwili na nusu iliyopita, Real Madrid ikamwamini. Ikampa timu hiyo tajiri zaidi duniani. Wakati huo Zidane alikuwa anatoka kuwa kocha wa kikosi cha vijana cha timu hiyo.
 
Back
Top Bottom