Umbo la figo/structure
Figo hutoa mkojo kwa kutoa uchafu wenye sumu na maji zaidi kutoka mwilini. Mkojo unaotengenezwa katika figo hupitia kwenye mrija uitwao” ureta, na huteremka hadi kwenye kibofu (bladder) na mwisho hutoka kupitia mrija wa urethra.
Watu wengi (waume kwa wake) wana figo mbili.
Figo ziko sehemu ya juu na nyuma ya tumbo, pande zote za uti wa mgongo (tazama mchoro) zinakingwa zisiathiriwe na mbavu za chini.
Figo huwa ndani kabisa mwa tumbo kwa kawaida mtu hawezi kuzihisi.
Figo ni viungo jozi ya umbo la aragwe lenye urefu wa sentimita 10, upande wa sentimita 6 na wembamba wa sentimita 4. Uzito wake ni kati ya gramu 150 – 170.
Mkojo unaotengenezwa kwenye figo huteremka hadi kwenye kibofu kupitia kwenye ureta.
Ureta ina urefu wa karibu sentimita 25 umbo la mrija uliotengenezwa kwa misuli ya kipekee.