Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nyota wa Manchester City, Leroy Sane ameachwa katika kikosi cha mwisho cha Ujerumani cha wachezaji 23 watakaocheza Kombe Dunia.
Kiungo huyo mwenye miaka 22, amekuwa katika kiwango bora katika kikosi cha Pep Guardiola na kufanikiwa kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora mwaka chipukizi ya PFA, lakini Joachim Low amemuona kama hafai katika kikosi chake cha Ujerumani kinachokwenda kutetea ubingwa wao Russia.
Kipa Manuel Neuer amekabidhiwa jezi yake namba 1 na atakuwa akianza pamoja na kuwa alikaa nje kwa miezi nane kutokana na majeraha ya goti.
 
Julian Brandt anaonekana kuwa ndiye aliyechukua nafasi ya Sane huku Julian Draxler na Marco Reus wakiitwaa katika kikosi hicho.
'Draxler, Reus na Muller wapo. Leroy ni mchezaji mwenye kipaji cha juu. Atarejea kikosini tena Septemba.'
Uamuzi wa kumuacha Sane, ambaye amefunga mabao 14 na kutegeneza magoli 15 msimu huu, limekuwa la kushangaza kwa jinsi Low alivyotazama uwezo wa chipukizi huyo.
 
Kikosi cha Ujerumani
Makipa: Manuel Neuer, Kevin Trapp, Marc-Andre ter Stegen.
Mabeki: Marvin Plattenhardt, Jonas Hector, Matthias Ginter, Mats Hummels, Niklas Sule, Antonio Rudiger, Jerome Boateng, Joshua Kimmich.
Viungo/ washambuliaji: Sami Khedira, Julian Draxler, Toni Kroos, Mesut Ozil, Marco Reus, Sebastian Rudy, Julian Brandt, Thomas Muller, Leon Goretzka, Ilkay Gundogan, Mario Gomez, Timo Werner.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…