Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

naweza kufikiri tofauti kidogo kutokana na wasomi na wengine wanavyofikiria siku hizi , tunaweza kubishana kuwa maisha hayana maana halisi , tupo tu kwa ajili ya kuzaa ili tuongezeke. Lakini hii sio maana halisi ya maisha.
 
Tunaweza kusema kuwa na dini fulani ili ufike mbinguni, maisha ni kujulikana, ni kujaribu kuifanya Dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi, lakini yote tunayofanya tunafuata mambo yale yale yaliopita zamani , mipango iliyopita, hata ufahamu wetu tulionao tunafikiri tuna uzoefu wa kitu fulani ndani ya vichwa vyetu ambavyo havijawahi kutokea, au vinatokea tu kama kivuli kwenye kazi za ubongo wetu. Ni kweli ndani yetu tuna vitu vikubwa lakini hatuelewi.
 
Mimi nafikiri ipo maana ya maisha lakini bado hatujaelewa, tunajiona kama tumetengenezwa na mashine au tunaishi kwa kutegemea mashine iliopo ndani yetu. Sidhani kabisa kama maisha hayana maana kati ya kuzaliwa na kufa kuna kitu mtu anatakiwa kukifanya ili aweze kufurahia maisha yake ya huo muda. Na hii sio kwa sababu mimi ni mtu wa dini sana hapana .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…