Kwa busara zangu nikaona bora nisiende,” alisema.
Alisema licha ya kwamba meya wa Iringa, alikuwapo lakini Kasesela hakutambua uwapo wake akamsimamisha mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Rita Kabati kama mbunge wa Iringa.
“Alipoona wananchi wamempinga hadharani, akaona bora anidhalilishe kwa kusema mimi sijatoa mchango. Mimi kama mbunge nilichangia kwa kupitia wabunge wa Mkoa wa Iringa, hii si mara ya kwanza kwa Kasesela kufanya hivyo akiwa jukwaani,” alidai.