Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Msiba wa Maria na Consolata Mwakikuti umeacha mzozo mkoani Iringa baada ya mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesela na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa kurushiana maneno.

Majibizano hayo yalianzia kwenye akaunti ya twitter ya Msigwa juzi, Juni 6 wakati wa ibada ya mazishi ya pacha hao (21) walioungana ambao waliofariki dunia Juni 2 na kuzikwa juzi katika makaburi ya Tosamaganga.

Katika majibizano hayo, Msigwa alimlalamikia Kasesela kuwa aliutumia msiba huo kisiasa na kushindwa kumtambua yeye na meya wa manispaa hiyo.
 
Katika akaunti hiyo Msigwa aliandika: “DC Kasesela anafanya siasa kwenye msiba wa Maria na Consolata. Bila aibu hajaacha kutaja jina langu akidhani kwa kufanya hivyo itamsaidia kisiasa. Kasesela usitumie huo msiba kwa faida ya kisiasa.

“DC Kasesela kila wakati is looking for attention! Kukiwa na harusi anatamani awe bwana harusi! kukiwa na ubatizo anatamani awe mbatizwaji! Kukiwa na msiba anatamani awe jeneza.”
 
Kasesela alimjibu Msigwa akisema: “Mheshimiwa mbunge is this Real you?! (Ni wewe kweli) Nimesema neno gani baya?”

Msigwa akamjibu: “Umesema mbele ya hadhara kuwa mimi sijatuma rambirambi ulijuaje? Kwani mimi nilipaswa kukupa wewe? Hao wabunge wa CCM hawajakwambia kama nilichangia! Kwani unadhani watu wa Iringa hawamjui mbunge wao?”
 
Msigwa alipoulizwa jana kuhusu majibizano yake na Kasesela alisema, DC huyo anatumia vibaya majukwaa kumdhalilisha. “Hana jema, niwepo au nisiwepo katika tukio la aina yoyote atatafuta sababu tu ya kunidhalilisha,” alidai.

Kuhusu kutohudhuria mazishi ya pacha hao wakati akiwa ni mbunge wa Iringa Mjini, alisema siku hiyo alikuwa na majukumu mengine aliyopaswa kuyakamilisha. Hata hivyo, alidai kuwa alipata taarifa kwamba kuna mipango ya mahsusi ya kutumia msiba huo kisiasa.
 
Kwa busara zangu nikaona bora nisiende,” alisema.

Alisema licha ya kwamba meya wa Iringa, alikuwapo lakini Kasesela hakutambua uwapo wake akamsimamisha mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Rita Kabati kama mbunge wa Iringa.

“Alipoona wananchi wamempinga hadharani, akaona bora anidhalilishe kwa kusema mimi sijatoa mchango. Mimi kama mbunge nilichangia kwa kupitia wabunge wa Mkoa wa Iringa, hii si mara ya kwanza kwa Kasesela kufanya hivyo akiwa jukwaani,” alidai.
 
Aliendelea, “Ni vyema Kasesela ajue kuwa siwajibiki kwake na hata nikitoa mchango au nisipotoa, siwezi kutoa taarifa kwake.”

Kasesela alisema hawezi kutumia jukwaa la msiba kumnufaisha mtu. “Nilipomtambulisha Mbunge Kabati kuna padri akauliza kuhusu Msigwa. Nikasema sifahamu kama yupo nipewe taarifa zake au rambirambi.”
 
Kasesela: “Omba re play you should not stress yourself nimegundua hukunisikia umeambiwa.”

Msigwa: “Nimekusikia watu walikushangaa sana unaposema eti Rita ni mbunge wa Iringa! Na walikupinga! Umeshindwa kumheshimu meya wa mji! Hata wewe hustahili heshima.”

Kasesela: “Sasa Rita Kabati ni mbunge wa wapi.”

Msigwa: “Acha ushamba”

Kasesela: “Mimi nimekubali ushamba toka jana kaka.”

Msigwa: “Kwa kweli washamba wanaviherehere!”
 
Msigwa alipoulizwa jana kuhusu majibizano yake na Kasesela alisema, DC huyo anatumia vibaya majukwaa kumdhalilisha. “Hana jema, niwepo au nisiwepo katika tukio la aina yoyote atatafuta sababu tu ya kunidhalilisha,” alidai.

Kuhusu kutohudhuria mazishi ya pacha hao wakati akiwa ni mbunge wa Iringa Mjini, alisema siku hiyo alikuwa na majukumu mengine aliyopaswa kuyakamilisha. Hata hivyo, alidai kuwa alipata taarifa kwamba kuna mipango ya mahsusi ya kutumia msiba huo kisiasa.
 
Kwa busara zangu nikaona bora nisiende,” alisema.

Alisema licha ya kwamba meya wa Iringa, alikuwapo lakini Kasesela hakutambua uwapo wake akamsimamisha mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Rita Kabati kama mbunge wa Iringa.

“Alipoona wananchi wamempinga hadharani, akaona bora anidhalilishe kwa kusema mimi sijatoa mchango. Mimi kama mbunge nilichangia kwa kupitia wabunge wa Mkoa wa Iringa, hii si mara ya kwanza kwa Kasesela kufanya hivyo akiwa jukwaani,” alidai.
 
Aliendelea, “Ni vyema Kasesela ajue kuwa siwajibiki kwake na hata nikitoa mchango au nisipotoa, siwezi kutoa taarifa kwake.”

Kasesela alisema hawezi kutumia jukwaa la msiba kumnufaisha mtu. “Nilipomtambulisha Mbunge Kabati kuna padri akauliza kuhusu Msigwa. Nikasema sifahamu kama yupo nipewe taarifa zake au rambirambi.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…