Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hispania ilitwaa taji hilo ikiwa imetenganishwa takriban kilometa 12 tu na linapoanzia bara la Afrika kwenye ramani. Licha ya wenyeji wa mashindano hayo Afrika Kusini kulikosa kombe hilo lakini walishangilia kwa nguvu ushindi wa Hispania katika fainali hizo zilizofanyika kwa mara ya 19.
 
Jambo jingine ambalo halitasahaulika kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika bara la Afrika, ni ukarimu na ucheshi wa wenyeji kwa wageni hasa kuwapa sapoti ya kushangilia mabingwa Hispania.

Hispania waliendeleza shangwe za ushindi wao kwenye dimba la Soccer City ambako ulikuwa ni uwanja zilipofanyika fainali hizo nchini Afrika Kusini.
 
Timu ya Taifa ya Ujerumani ndio mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014 wakichukua taji hilo kwa mara ya nne katika historia ya mashindano hayo.

Ujerumani iliiadhibu Argentina bao 1-0 katika muda wa nyongeza 120 likiwekwa wavuni na Mario Gotze zikiwa zimebaki dakika saba ngwe hiyo kukamilika.
 
Mchezo huo ulipigwa Maracana Rio de Janeiro nchini Brazil. Nyota huyo alithibitisha ubora wake mbele ya wachezaji wa Argentina, huku akiiongezea taji la nne ukijumlisha na yale ambayo imetwaa mwaka 1954, 1974 na 1990.

Ujerumani ilichukua kibabe kombe hilo mbele ya nyota wa Argentina wakimo Lionel Messi, Pablo Zabaleta na Philipp Lahm.
 
Mchezaji wa Argentina, Manuel Lanzini atazikosa fainali za Kombe la Dunia msimu huu wa kiangazi nchini Russia baada ya kupata majeraha.

Nyota huyo wa West Ham mwanzoni mwa mwezi Machi, Lanzini aliifungia timu yake ya bao la kwanza ilipokuwa ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Italia ambako iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
 
Taarifa rasmi ambayo imetolewa na Shirikisho la Soka Argentina, imeeleza kwamba mchezaji huyo amemepata majeraha kwenye mazoezi ya kikosi hicho leo Ijumaa asubuhi, hivyo atazikosa fainali za Kombe la Dunia Russia.

Lanzini amefunga jumla ya mabao 29 msimu uliopita kwenye klabu yake ya West Ham.
 
Argentina inayonolewa na kocha Jorge Sampoli ipo kundi D na itatupa karata yake ya kwanza kwenye fainali za Kombe la Dunia katika mchezo utakaowakutanisha na Ice Land Juni 16.

Pia itakuwa na mchezo mwingine dhidi ya Crotia Juni 21 na itashuka dimbani tena kumenyana na Nigeria Juni 26.
 
Mpaka ile avatar yako niliitamani
Pole bro...Ina maana hujabakiwa na chembe chembe zo zote za ugumu?[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Screenshot_20180608-131247.jpg
 
Back
Top Bottom