Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati nikiwa mdogo, mama yangu alipenda kunifundisha vitu vinne muhimu katika maisha ambavyo ni utu, utii, heshima na ukarimu.

Mara zote mama alipopata nafasi ya faragha ya kuzungumza na mimi, hakusita kuniweka wazi juu ya vitu hivi vinne.
 
Aliniambia,“Ukiwa mkubwa mwanangu penda kuwasadia watu kulingana na Mungu aatakavyokuwa anakubariki. Saidia wagonjwa na kila anayehitaji msaada wako bila kuomba malipo. Huo ndiyo utu. Watendee wema wageni wanaofika nyumbani kwako, kinyume na hapo utakuwa umekosa ukarimu. Mama hakuchoka kunifunza mwanawe, hata pale alipoona somo lake haliniingii akilini alitumia njia mbadala ya kuniadhibu ili tu nisijekosa hata kitu kimoja wapo kati ya hivyo vinne.
 
Mama aliniambia “Jitahidi mwanagu kuwaheshimu watu, haijalishi ni wakubwa kuliko wewe ama ni wadogo, masikini au tajiri. Unapokuta watu wamekaa, wasalimie kwa heshima. Ukiona mtu anayekuzidi umri amesimama mpe kiti akae, usitukane watu, usigombanishe watu. Zungumza na watu kwa utulivu, usipende kupayuka na kujifanya unajua sana. Mtu mkubwa anapokuambia jambo jema msikilize kwa makini na ikibidi tenda kama anavyokuelekeza, kama ni jambo jema na la msingi.
 
Hata hivyo, kadiri miaka inavyozidi kusonga, jamii inabadilika na mambo yanabadilika na kuwa kinyume ya tulivyozoea.

Zamani nilikuwa nikishuhudia dereva akizimikiwa na gari barabarani, wapita njia walikuwa wakisimama na kumsaidia bila kuomba chochote, Lakini kwasasa mambo ni tofauti. Gari yako ikiharibika hakikisha mfuko wako unasoma vizuri la sivyo utalala barabarani.
 
Zamani mtu akizama kwenye maji ama akipata ajali, watu walikuwa wakiwahi eneo hilo na kumpatia huduma ya kwanza bila kudai malipo yoyote. Zama hizi ataishia kupigwa picha hata akipewa msaada basi lazima kitolewe chochote na kama ni ajali ya gari, basi ataibiwa kila kitu kabla ya kupatiwa msaada.
 
Enzi zile, mtaani kukitokea msiba, nyumba zote na maeneo ya biashara nay a starehe yalikuwa yakifungwa na watu wanaenda kushiriki msibani.

Lakini siku hizi msiba umegeuka fursa kwa wengine. Unakuta nyumba ina msiba, ya pili wanapiga muziki mkubwa na wenye maduka, pub na baa wanafurahia kuwa siku hiyo watauza kwa kiwango kikubwa bidhaa zao. Zama zile mtu akipata msiba watu hukusanyana na kumfariji mfiwa. Zama hizi mtu anaondoka na kwenda kazini hata kama msiba upo jirani na mlango wa nyumba yake.
 
Vijana wakiume walikuwa wakifanya kazi ya kuchimba kaburi na kufanya kazi zote msibani na yeyote aliyeshindwa kushiriki alikuwa akitengwa au kuadhibiwa. Lakini dunia ya leo ya sayansi na teknolojia iliyojaa vijana na wazee wa kisasa, mambo yamebadilika. Yalianzia mijini na sasa yameingia hadi vijijini. Nilistaajabu nilipokwenda kijijini kwetu mwaka jana na kukuta kuna mabadiliko. Watu kwenda kwenye msiba wa jirani ni mpaka pawepo na video.
 
Biashara hiyo inazidi kushamiri na kila kukicha wengine wanajaribu kuvutia biashara hiyo kwa kukodisha magari yaliyotiwa nakshi mbambali kusudi tu, apate wateja wengi.

Binafsi najiuliza, huu ndiyo utu, heshima, ukarimu na utii tuliofundishwa na wazee wetu?

Nawasihi Watanzania wenzangu tubadilike, utamaduni huu tunaokwenda nao sasa si wa kwetu, hautufai tujaribu kurejesha wakwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…