Licha ya wazazi wake kuachana , familia ya Pogba ilikuwa na jukumu kubwa katika ukuwaji wake wa soka , ikiwa na hamu kubwa na mchezo huo wakati alipojiunga na klabu yake ya kwanza Roissy-en-Brie, klabu hiyo ilikuwa maili chache kutoka nyumbani kwao.
Sambou Tati, rais wa klabu ya Roissy-en-Brie: "walilazimika kumpatia mahitaji yake yote kama vile wazazi wazuri wangemfanyia mwanao. Paul alikuwa kitinda mimba ambaye alihitaji mamake kila mara , hivyobasi mamake alimtelekeza kama vile alivyowafanyia pacha. Lakini huku Paul akiwa mdogo ,kweli, wakati unapokuwa kitinda mimba mara nyingi utashughulikiwa sana. Wazazi wake walimpenda sana.