Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

hahaha [emoji23][emoji23][emoji23] i lost a caption of this out of laughing my bandama out [emoji23][emoji23][emoji23]

Can you CAPTION this...
5afd83b798c6e_HxIosjZ__700.jpg
 
Aliivutia klabu ya Le Havre
Pogba huenda alivutia wengi alipokuwa akiichezea klabu yake ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 13 lakini hakuitwa katika kituo cha kufunza soka ya kitaifa cha Clairefontaine national football .
Hatahivyo, klabu inayocheza soka ya kulipwa ya Le Havre ilikuwa tayari imeanza kuchunguza kipaji cha mchezaji huyo kupitia klabu ya Torcy, ikamsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 14 katika shule ya kufunza soka.
Franck Sale, Mkuu wa kitengo cha usajili wa wachezaji katika klabu ya Le Havre: "Nilisikia kuhusu Pogba katika kitongoji cha Paris kutoka kwa wenzangu ambao walimuona wakati alipokuwa mdogo akiwa na umri wa kati ya miaka 11 na 12 , hivyobasi tulienda kumuona mara moja. Alikuwa akicheza katika uwanja wa City Stade tuliona ujuzi wake na baadaye tukaenda kuona akicheza katika uwanja mkubwa .Paul tayari alikuwa akicheza na vijana wakubwa. Kulikuwa na klabu nyingi zilizokuwa zikimhitaji lakini ni chache ambazo zilipata fursa kumuona akicheza. Tulimgundua mapema. Kwa kweli PSG ilimuona kwa sababu alikuwa katika vitongoji vya Paris.
Alipokuwa akiondoka nyumbani kwao
 
Ilimchukua muda wa saa moja na nusu kwa Pogba kusafiri kutoka nyumbani kwao hadi makao makuu ya shule ya mafunzo ya soka kutoka Paris. Hatahivyo safari hiyo haikumkwaza kijana huyo ambaye alijawa na hisia alipokuwa uwanjani.
Sale: "ilikuwa vigumu kwake kwa kuwa alikuwa na ari ya kuwa mchezaji wa kulipwa na kwa sababu Paris na Havre haziko mbali. Angeweza kwenda nyumbani kwa urahisi na ilikuwa rahisi kwa familia yake kumtembelea , lakini alikuwa na malengo hadi hatuwezi kusema kwamba alivunjika moyo kwa kuiwacha familia yake -ilikuwa rahisi kwake.
'Tulimsukuma kufanya bidii zaidi'
 
Haikuwa rahisi kwa kiungo huyo wa kati katika klabu ya Le Havre. Pogba alikuwa na kipaji na ujasiri katika kazi yake , lakini wakufunzi wake walimtaka kufanya bidii zaidi ili kuafikia malengo yake ya ufanisi. Sale: "Alikuwa akifanya bidii sana lakini haikuwa rahisi kwa wakufunzi kwa sababu mara nyengine alionekana kuwa mjeuri. Tunazungumzia kuhusu hisia za kujiona muhimu mara nyengine ambazo bado zinaonekana katika tabia yake katika mechi fulani. Alikuwa na bidii lakini tulijua anaweza kujibiidisha zaidi na ndio maana tulimsukuma kufanya hivyo.
Alionekana nchini Scotland, akielekea Manchester United.
 
Pogba alivutia timu nyingi alipojiunga na timu ya taifa ya Ufaransa yenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 16. Mabingwa wa Itali Juventus, walikuwa na hamu naye kama vile Manchester United baada ya Pogba kuiwakilisha timu yake katika michuano ya vijana katika ziara ya Scotland. Pogba aliamua kujiunga na Man United huku Fifa ikiunga mkono mkataba huo mwezi Octoba 2009 baada ya mgogoro kati ya United na Le Havre kuhusu kandarasi yake.
 
Sale: "Nilikuwa tayari nimewaonya wakuu wangu kwamba ni hatari kuwawacha wachezaji wetu vijana kwenda katika zitra kwa kuwa vilabu vya Uingereza vinawachunguza sana. Nikiwa mtu niliyejua kuhusu kipaji chake, sikushangazwa hata kidogo kwamba Man United walikuwa wana hamu naye. Lakini kulikuwa na klabu nyengine nyingi ambazo zilikuwa zikimnyatia. Ilituvunja moyo sana kama wakufunzi , kwa sababu tulitaka kumuingiza katika timu ya wachezaji wa kulipwa . Wakati huo kandarasi yake ilikuwa wazi ndiposa United wakachukua fursa hiyo.
 
Back
Top Bottom