Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

446412323_140797.jpg
 
Moja ya story ambazo sikuwahi kufahamu ni juu ya hizi sheria za jamii mbalimbaliduniani ambazo zinaweza kushtua kushangaza wengi wanaozisikia, kuzisoma ambapo kwa wale waliobahatika kuzitembelea sehemu hizi, basi ni mashuhuda…
 
Sudan
Katika nchi ya Sudan, hasa katika kabila laLatuka, kama mwanaume anataka kumuoa mwanamke, anamteka. Mwanaume huyo anaweza kuomba ruhusa ya baba kwanza ambaye kama atakataa, atalazimisha kumuoa mwanamke.
 
Ujerumani
Kabla ya ndoa nchini Ujerumani, hufanywa kwanza sherehe ya polterabend. Ni sherehe ambayo hufanywa na wanandugu kwa kutupa uchafu sehemu ambayo patafanyika harusi ili wanandoa wapafanyie usafi. Kitendo hiki kinatafsiriwa kuwa ugumu wa maisha watakayoishi kwenye ndoa. Panaweza kutupwa chochote isipokuwa vioo.
 
Brazil
Katika kabila la Satere-Mawe, Brazil, mtoto wa kiume anapotimiza umri wa miaka 12, atakuwa mwanaume kamili kwa kuweka mikono yake sehemu maalumu iliyowekwa siafu ambao watamng’ata kwa dakika 10.
 
Ugiriki
Ugiriki, ni lazima kwa wagiriki kusema“piase kokkino” watu wawili wanapotamka neno moja kwa wakati mmoja. Kitu kama hicho hutokea kama mtu atamuona paka mweusi: atalazimika kutema mate mara tatu. Kama hatofanya hivyo, kitu kibaya kitamtokea.
 
Back
Top Bottom