Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sio tu kwamba ataku-miss, bali pia itakupa fursa ya kuwa mbali naye. Mkitumia muda wote wa 24/7 kuwa pamoja haliwezi kuwa jambo zuri, na halitokuwa na afya kwenye uhusiano wa ndoa yenu. Anaweza kuwa na hisia za kudumaa au kuhisi kuwa hawezi kufanya vitu anavyopenda kuvifanya. Mnapopata fursa ya kuwa mbalimbali kwa saa kadhaa inawapa fursa ya kuungana tena baadae mkiwa na nguvu mpya.
 
Kutenga muda wa kukaa pamoja.
Wakati fulani tunashughulishwa mno na shughuli za maisha na utafutaji kiasi kwamba hatutengi muda kwa ajili ya wenza wetu. Ili kuwa na furaha ni muhimu kutenga muda maalum kwa ajili yake tu, hata kama ni dakika chache. Pia wekeni muda maalum kila wiki kwa ajili ya kunong'onezana ambapo hakuna watoto, hakuna marafiki au kitu kingine chochote, ni nyinyi wawili tu. Kumbushieni mahabba yenu na ladha ya muunganiko wenu.
 
Pia ni jambo zuri kutenga dakika kadhaa kila siku kwa ajili ya kuwasiliana. Mnaweza kutumia muda huo kujadili siku yenu inavyoendelea au kuchombezana. Kuwa na utaratibu wa kutenga muda maalum wa kuwasiliana au kuwa pamoja utaupa nguvu uhusiano wenu na kukufanya kuwa mwenye furaha.
 
IMG-20180608-WA0014.jpg
 
Back
Top Bottom