Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Miongoni mwa waliotajwa na Duale bungeni ni Jawasant Rai ambaye ni bwanyenye wa enzi za utawala wa Rais mstaafu, Daniel arap Moi.

Rai na familia yake pia ni rafiki wa familia ya Rais Uhuru. Kwa kuleta jina la hilo, Duale alitaka kulipiza kisasi baada ya Wasomali na washiriki wa karibu wa Ruto kuhusishwa na uagizaji haramu wa sukari.
 
Lakini, kama Duale alifikiria kwamba hatua yake ingewashtua wengi, basi aliambulia patupu. Msemaji mkuu wa Serikali, Eric Kiraithe alipuuzia mbali hatua ya Duale akisema ni porojo tupu.

Uhuru, Ruto njia tofauti

Kuna mgawanyiko unaotokota na utaendelea kuwa kidonda sugu kwa siku zijazo. Rais hajatishwa na hayo na ameapa kuendelea na operesheni hiyo hadi Kenya isafishwe kutokana na dosari za ufisadi na visa vingine vinayoathiri maendeleo.
 
Ingawa Ruto hajawahi kumkashifu Rais Uhuru hadharani, kuna kila sababu ya kuamini kwamba, kiongozi wa nchi hafurahishwi na mdogo wake.

Walipoingia mamlakani 2013, wawili hao walikuwa marafiki wa chanda na pete. Walivaa suti zinazofanana. Tai zao pia zilifanana. Hali hii iliendelea hadi Rais Uhuru alipoingia muhula wa pili na wa mwisho.
 
Hayo sasa ni historia. Rais na Ruto sasa wanatembea kwenye njia tofauti. Kila mmoja akiimba pambio lake.

Wiki tatu zilizopita, Rais alisema makamu wake ana mazoea ya “kutangatanga vichochoroni.” Matamshi haya ya Rais yalituma ishara kwamba mambo si sawa katika ngome ya Jubilee.

Rais ameacha kumtaja naibu wake kwa jina ama kumuita “ndugu yangu’ jinsi walivyokuwa wanaitana kwa muda mrefu.
 
Ruto na wafuasi wake hawaoni lolote kizuri katika juhudi za Rais. Baada ya kusema salamu kati yake na Raila zilikuwa na nia mbaya kwake, hawasiti kudai kwamba vita dhidi ya ufisadi ni mpango wa kumzima kisiasa.

Sasa ni vita vya sukari na tayari wanapiga nduru.

Wadadisi wa siasa wanasema masahibu ya Ruto yameanza tu na hivi karibuni mengi yatamtembelea.

Ruto ajidhatiti

Lakini, Ruto pia anapigana kufa kupona. Tayari ameanza kampeni za 2022 na yuko mbioni kutafuta wanasiasa watakaomsaidia kutimiza ndoto yake.
 
Hivi majuzi mbunge Moses Kuria alisema Wakikuyu hawana budi kumuunga mkono Ruto 2022 la sivyo watakuwa wanajitafutia laana.

Kuria ambaye ni mbunge wa eneo analotoka Rais Uhuru amesisitiza kwamba atahakikisha Ruto anapigiwa kura na zaidi ya watu milioni moja kutoka jimbo la Kiambu.

Katika eneo la Kenya ya Kati ambapo Rais Uhuru anajivunia kama ngome yake, wabunge wengi wameapa kusimama kidete na Ruto hadi 2022 liwe liwalo.
 
Pia, Ruto amewavutia katika upande wake wabunge takriban wote wa ODM katika Pwani. Hatua hiyo ya makamu wa Rais imeghadhabisha chama hicho kinachoongozwa na Raila.

Kinara wa walio wachache bungeni, John Mbadi na Katibu wa ODM, Eliud Sifuna wamewaonya vikali wabunge na maseneta wa ODM wanaotembeatembea na Ruto katika ziara zake za Pwani.
 
Miongoni mwa wabunge hao ni mbunge mbishi wa eneo la Bunge la Malindi, Aisha Jumwa. Licha ya kupokea onyo kwamba angeadhibiwa kwa kutangaza kwamba sasa anampigia debe Ruto, Jumwa ameapa kwamba hakuna lolote litakalomtisha.

Tayari ODM iko katika harakati za kumuondoa mbunge huyo kutoka Tume ya Huduma ya Bunge (PSC). Chama cha ODM kilifanya juu chini kuhakikisha kwamba Jumwa anaingia kwenye tume hiyo na wabunge wengine wawili wa chama hicho. Lakini sasa, kitumbua kimeingia mchanga na lazima aadhibiwe iwe liwe funzo kwa wengine wenye tabia ya kukaidi matakwa ya vyama vyao.
 
Wanasiasa wanafaa kuheshimu vyama vyao na pia kuenenda kuambatana na kanuni za vyama vyao. Ikiwa mbunge, seneta au gavana anaona kwamba kamwe maazimio yake kisiasa hayaambatani tena na nyenzo za chama chake, ana huru wa kujiuzulu rasmi na kutafuta fursa nyingine kwa kutumia tikiti ya chama ambacho amehamia.

Huwezi kuhamia chama kingine na kuanza kuwatukana watu ambao walikufanyia kampeni na wakasimama na wewe hadi ukaingia bungeni. Hiyo ni kama kujitia kitanzi.
 
Jumwa na wenzake wanadai wanamuunga mkono Ruto kuonyesha kwamba salamu kati ya Rais Uhuru na Raila zimezaa matunda.

Huu upuuzi mtupu

Salamu kati ya viongozi hao wawili haimaanishi kwamba wabunge wa ODM sasa wako huru kumangamanga kwa kila chama. Nani ameona Raila akisema anamuunga mkono kiongozi yeyote wa Jubilee kisiasa? Hamna.

Pamoja na hayo, Makamu wa Rais ametafuta uungwaji mkono kutoka kwa aliyekuwa mwaniaji wa urais, Peter Kenneth.
 
Akizungumza kwa mafumbo, Kenneth alisema mwishoni mwa wiki kwamba dalili ya mvua ni mawingu na hivi karibuni ushirikiano wake na Ruto utazaa matunda.

Huenda Kenneth akawa mgombea mwenza wa Ruto lakini hii inaweza kuleta mzozo kwa sababu wanasiasa wa Magharibi mwa Kenya wanategea mmoja wao achukue nafasi hiyo.

Pia, Pwani haitafurahishwa ikiwa wataachwa nyuma na Makamu wa Rais 2022. Wao wangetaka pia kutoa mgombea mwenza.

Raila alidokeza juzi kwamba ODM itapigania kiti cha urais 2022.
 
Vita vya jinai

Huku siasa ikiendelea kupamba moto, kikosi cha jinai nchini kinaendelea kuchunguza jinsi mabilioni ya maguni ya sukari yaliingizwa nchini kimagendo.

Pia, vita vya rais dhidi ya ufisadi vinaendelea ingawa kuna watu fulani wanaofanya kila wawezalo kuhakikisha haviendi mbali.

Je, Rais Uhuru ataamuru jamaa wake waliotajwa katika sakata za ufisadi wanaswe? Hadi sasa, mpwa, mjomba na dadake Uhuru ni miongoni mwa mamia wa Wakenya waliotajwa katika visa vya ufisadi.
 
Ni vema kwamba, uadui unaokithiri miongoni mwa viongozi wa jubilee umesaidia mno katika vita dhidi ya ufisadi. Kwa vile wanajuana kwa vilemba, vikundi hivi vinachimbana usiku na mchana na kufichua mafisadi kati yao.

Ni ombi la Wakenya kwamba waendelee kupigana hadi siri zao zote zitoke kwani hasira za mkisi, furaha ya kunguru.
 
[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Ushaanza kuwachokoza eenh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…