Mjadala mkali unaendelea nchini Tanzania kuhusu mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018 /2019 kuhusu zao la korosho. Mapendekezo hayo ni pamoja na kuondolewa kwa ruzuku ya asilimia 65 iliyokuwa inaenda kwenye Mfuko wa Maendeleo wa Korosho na badala yake, iende kwenye mfuko mkuu wa serikali.

"Haya mabadiliko ya sheria ya matumizi ya fedha yaani, finace bill, hatuyaungi mkono mpaka pale ambapo bunge litakapofanya uamuzi," hayo ni kwa mujibu wa Nape Nnauye ambaye ni mbunge wa jimbo la Mtama lililopo kusini mwa Tanzania.
Mjadala huo, unaonekana kugusa zaidi hisia za wabunge hasa wa mikoa ya kusini ambao moja kwa moja wametoafikiana na mpango huo. Wakati huo huo, hofu kubwa imetanda miongoni mwa wadau wa kilimo cha korosho.
Mahamud Seleman Lupanda, ni mkulima wa korosho kutoka Mtwara mjini anasema kilio chao haswa ni pembejeo, mara ya kwanza walikuwa wanazipata kwa njia ya ruzuku lakini sasa ruzuku ikiondolewa upatikanaji wa pembejeo utakuwa wa shida sana.
Mkulima huyu aliogeza kusema kuwa kama pembejeo zitapatikana kwa bei nafuu na kuwepo kwa usimamizi mzuri, basi itakuwa sawa lakini usimamizi uliopo sasa sio mzuri.
"Mpaka leo hii sijalipwa kilo 5000 za korosho, wakulima tunalima na hatujapata fedha zetu kwa muda mrefu sasa na hilo ni tatizo sana. Tuna imani hizo korosho zimeshafika kwa wanunuzi na sisi hatupati pesa zetu na tunataka kuanza kuandaa shamba," amefafanua Mohamud.
Salum Muhidin ni msafirishaji na mnunuzi wa korosho katika minada mkoani Mtwara anasema mabadiliko ambayo serikali inataka kuweka yamekuwa na ukakasi .
"Nikiwa mkazi na mzawa wa Mtwara ambapo korosho nyingi zinatoka naelewa kuwa, kama mbolea ya salfa hakuna basi uzalishaji wa korosho utaathirika sana."