Kumbuka siku zote hakuna mafanikio rahisi, hivyo ukiona magumu, changamoto zinakuwa nyingi utambue mafanikio yapo karibu, tena inawezekana hatua chache kutoka hapo ulipo, inua mguu, piga hatua uyafikie.
Wahenga walisema “Giza la usiku linapokuwa nene sana ujue alfajiri imekaribia”.
Uvumilivu iwe silaha kuu, usisahau kuwa na mtizamo chanya kwa kila unalotaka kufanya, usitangulize haiwezekani kwa sababu kila jambo linawezekana kwa bidii, maarifa, uvumilivu na kujituma, wakati unafanya hayo pokea ushauri wa maana achana na wanaokukatisha tamaa, angalia unataka kupata nini katika hilo jambo unalofanya.