Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Beki Sergio Ramos amesema hatastaafu soka ya kimataifa licha ya Hispania kung’olewa katika Fainali za Kombe la Dunia.

Nahodha huyo alisema anatarajia kucheza Fainali za Kombe la Ulaya zilizopangwa kuchezwa nchini England.
 
Pia, alisema ndoto yake ni kucheza Fainali za Kombe la Dunia zilizopangwa kuchezwa nchini Qatar mwaka 2022. Beki huyo wa kati mwaka 2022 atakuwa amefikisha miaka 36.

Ramos amekataa kufuata nyayo za mchezaji mwenzake nguli wa timu hiyo Andres Iniesta ambaye ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.
 
Mchezaji mwingine aliyetangaza kustaafu ni kiungo nguli wa Argentina aliyewahi kuwika Liverpool na Barcelona, Javier Mascherano.

Mshambuliaji nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo, amesita kuweka bayana mustakabali wake katika soka ya kimataifa muda mfupi baada ya timu hiyo kuondolewa katika fainali hizo.
 
Back
Top Bottom