Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kauli ya Ferdinand aliyewahi kucheza pamoja na Pique katika kikosi cha Manchester United iliungwa mkono na nahodha wa zamani wa England, Alan Shearer.

“Alipokosa mpira baada ya kuruka juu, aliona njia pekee ni kunyanyua mikono kuzuia. Alijua kabisa mpira uko juu ya kichwa, alifanya hivyo kwa kuwa tayari alikuwa amehamaki,” alisema Shearer.
 
Mshambuliaji Mohamed Salah amesaini mkataba mpya unaofanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Liverpool akipokea pauni 200,000 kwa wiki.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri kwa sasa yupo mapumzikoni baada ya Kombe la Dunia, lakini amemaliza utata wote kuhusu hatma yake ndani ya Liverpool kwa kusaini mkataba huu.
 
Kocha Jurgen Klopp tayari ameweka wazi kuwa lengo lake ni kufanya zaidi ya msimu uliopita ambao walicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa pamoja na kumaliza katika nne bora ya Ligi Kuu England.

Imekuwa ni jambo lilisubiriwa kwa muda mrefu na Liverpool kumalizana na Salah haraka baada ya kiwango chake cha juu msimu uliopita.
 
Mabao yake 32 katika ligi kuu yamevunja rekodi katika mechi 38 za msimu uliopita pia alikuwa na mchango wa kipekee kuisaidia klabu hiyo kufuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Real Madrid ambayo ilifunga Liverpool 3-1 jijini Kiev, wamekuwa wakihusishwa na kumtaka Salah kwa muda mrefu, lakini Liverpool mahusiano yao mazuri na wakala wa Salah, Ramy Abbas Issa na majadiliano mazuri na mkurungezi wa ufundi, Michael Edwards walimaliza kirahisi suala hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…