Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mchezaji mwingine aliyetangaza kustaafu ni kiungo nguli wa Argentina aliyewahi kuwika Liverpool na Barcelona, Javier Mascherano.

Mshambuliaji nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo, amesita kuweka bayana mustakabali wake katika soka ya kimataifa muda mfupi baada ya timu hiyo kuondolewa katika fainali hizo.
 
Tulipambana lakini imeshindikana. Lakini napenda kuendelea kucheza soka kwa miaka mingi zaidi kwa sababu nina uwezo,” alisema Ramos.

Nahodha huyo wa Real Madrid, alisema ataendelea kuitumikia timu ya Taifa kwa kuwa ana mapenzi ya kupeperusha bendera ya nchi hiyo.
 
Rio Ferdinand amemkangaa beki wa Hispania, Gerard Pique kwa kusababisha mkwaju wa penalti kwa timu yake.

Ferdinand alidai kuwa beki huyo wa kati alifanya makusudi kushika mpira huo ambao ulizaa bao la kusawazisha kwa Russia.
 
Nguli huyo ambaye ni mchambuzi wa soka, alisema Pique alicheza mchezo huo akiwa na hasira na hakushangaa kumuona akishika mpira ndani ya eneo la hatari.

“Alihamaki, unapojiona uko kwenye eneo baya unatakiwa kuwa makini, weka vizuri mikono yako. Uamuzi uliotolewa na mwamuzi ni sahihi,”alisema Ferdinand.
 
Kauli ya Ferdinand aliyewahi kucheza pamoja na Pique katika kikosi cha Manchester United iliungwa mkono na nahodha wa zamani wa England, Alan Shearer.

“Alipokosa mpira baada ya kuruka juu, aliona njia pekee ni kunyanyua mikono kuzuia. Alijua kabisa mpira uko juu ya kichwa, alifanya hivyo kwa kuwa tayari alikuwa amehamaki,” alisema Shearer.
 
Mshambuliaji Mohamed Salah amesaini mkataba mpya unaofanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Liverpool akipokea pauni 200,000 kwa wiki.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri kwa sasa yupo mapumzikoni baada ya Kombe la Dunia, lakini amemaliza utata wote kuhusu hatma yake ndani ya Liverpool kwa kusaini mkataba huu.
 
Salah, ambaye mkataba wake wa awali alikuwa akipokea pauni 100,000 kwa wiki wakati akitua Anfield akitokea Roma miezi 12 iliyopita, sasa anakuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi Liverpool akiwa amefunga mabao 44 katika mashindano yote.
 
Kocha Jurgen Klopp tayari ameweka wazi kuwa lengo lake ni kufanya zaidi ya msimu uliopita ambao walicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa pamoja na kumaliza katika nne bora ya Ligi Kuu England.

Imekuwa ni jambo lilisubiriwa kwa muda mrefu na Liverpool kumalizana na Salah haraka baada ya kiwango chake cha juu msimu uliopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…