Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

BchLlOjgVew.jpg
 
DIEGO GODIN
Beki mahili wa kati, kutinga robo fainali kwa Uruguay kuna mchango wake mkubwa. Kombinesheni yake na beki Jose Maria Gimenez anayecheza naye Atletico Madrid kumetuliza mizuka fowadi ya timu pinzani
 
Nahodha wa Nigeria ‘Super Eagles’, John Mikel Obi, ameitaka serikali kuimarisha ulinzi ili kupunguza matukio ya mauaji na utekaji nyara kwa ajili ya kudai fedha.

Kiungo huyo wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa anaitumikia klabu ya Tianjin Teda ya ya Ligi kuu ya China, aliyasema hayo siku chache baada ya kulipa kikomboleo kwa ajili ya baba yake mzazi aliyetekwa nyara.
 
Alisema kuwa alipata taarifa za kutekwa kwa baba yake akiwa Russia dakika chache kabla ya kuiongoza Nigeria kucheza na Argentina katika mechi ya mwisho ya kundi D.

“Kwa mara nyingine niliishi kwa hofu na wasiwasi, nikiogopa kumpoteza baba yangu ambaye alitekwa na kutakiwa alipiwe fedha ili aachiwe huru,” alisema Obi.
 
Back
Top Bottom