Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kiasi fulani, bahati hutegemea maarifa. Mtu mwenye maarifa hufanya kazi kwa uhuru. Ni vigumu kutenganisha bahati na maarifa; kwani ili kufanya kitu kwa usahihi uwezo wa mtu husika kufuata sheria na kanuni ipasavyo unahitajika.
 
Kwa kuwa bahati hutegemea imani, mtu anapaswa kuwa makini na kiwango cha imani yake wakati anapofanya jambo lolote lile. Ikiwa kama kiwango cha imani ni kidogo, yafaa kusitisha kufanya jambo hilo, au kufanya hatua kwa hatua na kwa umakini mkubwa kama haiwezekani kusitisha shughuli husika.
 
Watu wanaolazimisha kufanya jambo bila ya imani nalo hujikuta wakifanya makosa bila ya kujitambua, kusahau hatua za kufuata, kushindwa kujitetea pindi wanapotakiwa kijitetea, hivyo kubaki wakijilaumu kwa kujisemea "nina bahati mbaya".
 
Kukosa umakini kimawazo huwafanya watu kudharau mambo ya msingi; kujikuta wakifanya mambo wasiyotayatarajia kisha kutokufanikiwa. Ili kuongeza nafasi ya bahati ya kufanikiwa yapaswa kuwekeza kimawazo, kushirikisha maarifa kwenye kazi ifanyikayo kwa wakati husika. Kuwekeza kimawazo husaidia kutumia rasilimali kwa ufanisi zaidi.
 
ROBIN OLSEN
Golkipa huyu huyu Sweden ameonyesha uwezo mkubwa kuwazuia Ujerumani, na kadri timu ya Sweden inavyosonga mbele anaonyesha kipaji cha juu kwenye milingoti mitatu ya goli lake. Mafanikio ya taifa la Sweden mpaka sasa yana mchango wake mkubwa
 
Takribani watu wote (wanasayansi mashuhuri, wafanyabiashara wakubwa, wasomi n.k) waliofanikiwa, walifanikiwa kwa kuwa kiwango chao cha imani kilikuwa juu. Kufanya kazi bila ya i tiketi ya kushindwa. Mtu anayetaka bahati nzuri huchagua mtizamo chanya, mtizamo chanya huongeza nishati na kusadia jitihada za kufanikiwa.
 
Kila mtu anayo nafasi ya kufanikiwa, watu wengi hawajui maana na jinsi ya kulinda nafasi wanazopata katika maisha. Bahati nzuri ipo, na kila mtu anao uwezo wa kuitawala. Kwa kulitambua hilo, hakuna haja ya kuogopa kufanya jambo lolote kwa kuwa hakuna bahati mbaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…