Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mechi za Kombe la Dunia, mechi ya kwanza Iceland ilitoka droo na Argentina ndio nikaanza kuona sasa zile kanda zikianza kusambaa mitandaoni kila mahali na hapo ndipo watu walianza kuuliza kwamba nilisema Messi atakuwa mshindi kwenye Kombe la Dunia sasa wanatazamia ahadi yangu itimie.''
 
Mechi ya pili Croatia ikafunga magoli matatu wakasema ahh…aga mapema basi acha kazi ulitwambia kwamba Messi asipochukua Kombe la Dunia utaacha kazi yako''
"Hapo ndipo nilipoanza kupingana na umma, raia walikuwa wakisema Messi akitoka ondoka.
Kwa hivi sasa nitaacha kazi yangu."
 
Joe anasema kwamba hii si mara yake ya kwanza kutoa ahadi kama hiyo.
''Kuna wakati nilitoa ahadi nilipokuwa msemaji wa timu ya Sunrise ya daraja la kwanza nikasema Espoir haiwezi kuishinda mechi mbili, ikinishinda mechi mbili mfululizo mimi nitaiacha kazi hiyo," anasema.
 
Na kwa kweli Espoir ilijitahidi na wakanifunga mechi ya pili kwa hivyo tangu siku hiyo nilitoka kwenye Sunrise lakini ni ahadi niliongea hata mimi mwenyewe sikutarajia kama itafika hapa na kusambaa mitandaoni kama hivi."
Lakini kama kawaida yangu ndio hivyo michuano ya Kombe la Dunia inamalizika tarehe 15 Julai.
"Nitakuwa nimemalizika miaka tisa kwenye hii kazi ya kutangaza mpira na vipindi mbalimbali vya michezo basi nitaiweka chini niendelee na mambo mengine."
 
Beki wa Brazil Danilo hatacheza tena Kombe la Dunia nchini Urusi baada yake kuumia kwenye kifundo cha mguu akifanya mazoezi Alhamisi.
Mchezaji huyo wa Manchester City aliumia mkesha wa mechi muhimu kwa Brazil robofainali Kombe la Dunia dhidi ya Ubelgiji.
Mechi hiyo itaanza saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Kazan Arena mjini Kazan.
Mchezaji huyo aliumia kwenye kano zilizo kwenye kifundo cha mguu wake wa kushoto.
Ingawa hatarajiwi kucheza tena, ameombwa kusalia na kikosi Urusi.
 
Danilo, 26, aliwachezea Brazil mechi moja pekee ambayo walitoka sare 1-1 na Uswizi mechi yao ya kwanza 17 Juni na kisha akaumia kwenye misuli ya paka.
Nafasi yake katika kikosi cha kuanza mechi Brazil imekuwa ikijajwa na beki wa kushoto anayechezea Corinthians, Fagner.
Danilo alikuwa ameitwa kwenye kikosi kujaza nafasi ya beki wa Paris St-Germain Dani Alves, ambaye alikosa michuano ya mwaka huu kutokana na jeraha la goti.
 
Kiungo wa kati Casemiro amesimamishwa kucheza kutokana na kupata kadi mbili ya manjano na nafasi yake itachukuliwa na Fernandinho, kwa mujibu wa kocha wao Tite.
Beki wa kushoto Marcelo ambaye hakuwa sawa kabisa mechi yao ya mwisho amepona tatizo la mgomo na atachukua nafasi yake kutoka kwa Filipe Luis.
Winga Douglas Costa pia amepona jeraha la misuli.
 
Mechi moja mabao saba, Lukaku na Hazard kufufuka na kuitoa Japan, nayo Uingreza kushinda kwa penalti mara ya kwanza.
Kombe la Dunia la kuvutia zaidi nyakati hizi linaingia hatua ya robo fainali. Hapa tunaangazia tunayotarajia kwenye mechi nne zitakazoamua atakayeingia nusu fainali ikiwemo mfaransa anayeipenda Uruguay lakini hana budi kuwatema nje....
'Mfaransa mpenda Uruguay anayesaka kuwatoa marafiki zake'
 
Ni Urafiki kando, kazi kwanza wakati straika wa Ufaransa Antoine Griezmann atacheza dhidi ya rafiki zake ambao ni walinzi wa Uruguay, Diego Godin na Jose Gimenez, wanaoitumikia klabu ya Atletico Madrid.
Baada ya Uruguay kujikatia tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia, ni Griezmann ndiye alienda uwanja wa ndege wa Madrid kuwapokea wachezaji wake waliorejea, Godin na Gimenez, huku akiwa amevaa jezi ya Uruguay.
Griezmann amesema anahisi kuwa "Muuruguay wa kuchanganya".
"Ni uraia ninaoenzi, taifa linalopenda na mechi hii itakuwa ni ya hisia nyingi kwangu."
 
Lakini Luis Suarez, mfungaji wa Uruguay anayepiga timu ya Barcelona anapinga kauli hii.
"Ni mfaransa na hafahamu kuwa Muuruguay inamaanisha nini," alisema Suarez.
"Hatujui sisi ni kina nani au ni nini tunapaswa kufanya ili tufanikiwe kwenye soka.
Anajivunia tamaduni zetu, na anazungumza lugha sawa- lakini tunahisi namna tofauti."
 
Achia mbali mapenzi ya Atletico Madrid,mchuano unatarajiwa kuwa mkali na wa ajabu.
Mtaifa yote yamejihami kwa washambulizi matata ulimwengu wa soka na wote wamewaondoa mataifa tajika kwenye soka hatua ya mchujo.
Ufaransa inajigamba kuwa na watatu kati ya wachezaji watano ghali mno duniani punde tu uhamisho wa Kylian Mbappe wa euro milioni 180m (£159m) kutoka Monaco hadi Paris St-Germain utakapokamilishwa.
Mbappe alikuwa chipukizi wa kwanza kuyatandika magoli mawili tangu gwiji wa zamani wa Brazil, Pele, timu yake ya Ufaransa ilipowanyoa Lionel Messi na Argentina 4-3 mechi iliyopita.
Uruguay - iliyowakung'uta Ronaldo na Ureno - inajidai kwa kuwa na Suarez na Edinson Cavani ambaye ni mfungaji mwenye mabao Zaidi historia ya Paris St-Germain, kwenye safu ya ufungaji. Wawili hawa wana jumla ya mabao 98 ya kimataifa.
Ubelgiji kujutia kuizima Uingereza?
 
Ubelgiji huenda inajutia kutua kwenye upande mgumu wa mechi zilizosalia Kombe hili kwa kunyakua nafasi ya kwanza kundi G.
Walitoka nyuma 2-0 na kuwalisha upanga Japan katika ngarambe kali Jumatatu - ilikuwa timu ya kwanza kuandikisha matokeo aina hiyo tangu 1970 - lakini wamezawidiwa kwa kukutanishwa dhidi ya timu inayopigiwa upatu kuinua Kombe mwaka huu na walioliinua mara tano kufikia sasa - Brazil.
Ingefungwa na Uingereza, Ubelgiji haingepata pingamizi kuinua kombe hilo la dhahabu tarehe 15 Julai.
Ubelgiji - isiyopoteza mechi 23 mpaka sasa - ndio moja kati ya timu mbele pekee Urusi kushinda mechi zake zote nne ilizocheza.
 
Wamefichua makali yao dhidi ya Japan na kuwanyamazisha wakosoaji wake waliotilia shaka uwezo wao wa kuwaangamiza wapinzani walipowadhalilisha Japan huku mlango wa kutokea ukiwakodelea macho na kutishia kuwanyima nafasi ya robo fainali.
"Tulipokuwa nyuma 2-0 dhidi ya Japan tulihisi kisaikolojia kuwa 'Sawa, hatuna la kupoteza',hilo lilituweka huru," alisema kocha wa Red Devils Roberto Martinez
 
Hili tutalidumisha dhidi ya Brazil, ila tu hisia hizi zitakuwa kuanzia sekunde ya kwanza."
Huu ndio mchuano utakaoshuhudia wengi wa mastaa waliosalia Urusi Kufikia sasa - Barcelona, Chelsea, Liverpool, Manchester City na Paris St-Germain watawakilishwa na angalau mchezaji mmoja.
Neymar ni mmoja wa wachezaji wa kupendeza ngarambe hizi - Ingawa sio kwa kila jambo.
Amesajili mabao mawili Urusi - lakini sarakasi zake pindi anapoumia,zimemletea kejeli kutoka mashabiki.
Ingawa safu ya ushambulizi ya Brazil ndio imepokea sifa nyingi, mabeko wao pia wanastahili kongole kwani wamefungwa bao moja tu katika mechi tisa walizocheza. Aidha, katika Kombe la Dunia Urusi wameruhusu shuti tano tu kwenye lango lao.
 
Back
Top Bottom