Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

STRAIKA, Pierre-Emerick Aubameyang hakutaka kusubiri hadi msimu mpya wa Ligi Kuu England uaze ndio amvutie kocha wake mpya, Unai Emery baada ya kufanya hivyo kwenye siku ya kwanza tu ya kuanza mazoezi,
Staa huyo wa kimataifa wa Gabon ana miezi sita tu kwenye kikosi cha Arsenal, lakini mambo yake yanazidi kunoga kila siku jambo linalowafanya mashabiki wa timu hiyo kuamini katika huduma yake kwamba itawafanya watambe msimu ujao.
 
Kwenye mechi za ligi alizocheza msimu uliopita, Aubameyang amefunga mabao 10 na kuasisti manne katika mechi 12 alizoanzishwa kwenye ligi hiyo. Na sasa ameweka rekodi kwenye klabu hiyo ya Emirates baada ya kuruka kwa mita 7.97 kwa mguu mmoja, jambo ambalo halijawahi kufanywa na mchezaji yeyote kwenye timu hiyo wakati walipokuwa wakifanyiwa mazoezi ya viungo kutambua ufiti wao kabla ya maandalizi ya msimu mpya kuanza.
 
Kocha, Emery alivutiwa na ubora huo wa Aubameyang na kuamini kwamba msimu ujao utakuwa mtamu kweli kweli hasa kwenye mpango wake wa kutaka kuwashindanisha washambuliaji wawili na Alexandre Lacazette kuleta kitu kizuri kikosini.
 
ANTONIO Conte ameripotiwa amebakiza hatua chache tu kuufikia mlango uliandikwa maneno 'exit' huko Stamford Bridge baada ya Chelsea kukaribia kabisa kukamilisha dili la kumnasa kocha mpya.
Wachezaji wa Chelsea ambao hawapo kwenye fainali za Kombe la Dunia wanatarajia kuwasili Cobham wikiendi hii ili kujiandaa na mazoezi yatakayoanza rasmi Jumatatu, huku kocha Conte akitarajia kuwapo pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…