Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

WAKATI ule mtindo wa wanasoka mastaa wa kutoka na warembo wanamitindo au waigizaji ukionekana kubamba zaidi, utashangaa kuna wanasoka wengine wao wala hawangaiki na mapenzi.

Hawafagilii kabisa masuala hayo kwa maana hawana wachumba. Wanachojua wao ni kufanya mambo yao ndani ya uwanja tu na si vinginevyo. Jamaa hao hawa hapa.
 
Romelu Lukaku

Mwaka 2014 kwenye kipindi cha majira ya kiangazi, Romelu Lukaku, alionekana akifurahia likizo yake na mtoto mmoja mkali hivi, Julia Vandenweghe.

Lakini, tangu mwaka 2015, Lukaku anadaiwa kuwa singo. Ilidaiwa kwamba sababu ya Lukaku kuachana na mpenzi wake ni kutokuwa na mpango sana wa kufuatilia masuala ya kimahaba kwani muda wote akili yake ipo kwenye mchezo wa soka.
 
N’Golo Kante

Kiungo mkata umeme wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, N’Golo Kante, yupo singo na hajawahi kuwa na mwanamke yeyote huko nyuma.

Licha ya kuwa maarufu, N’Golo, hataki kabisa kuzungumzia maisha yake binafsi na kwamba muda wote amekuwa akiwekeza akili yake kwenye kazi yake ya kucheza mpira. Kutojihusisha na wanawake pengine ndilo jambo linalomfanya kiungo huyo kuwa na mapafu ya mbwa uwanjani akicheza bila ya kuchoka kwa dakika zote.
 
Diego Costa

Straika, Diego Costa, alishawahi kuwa na mpenzi, lakini uhusiano wao ulivunjika baada ya mrembo huyo kumshutumu kwamba alitoka na dada yake na kisha rafiki yake.

Kwa maana ya Costa amesaliti kwa kutoka na dada na rafiki wa karibu wa mwanamke huyo, Michele Zouanne. Uhusiano wao wa kimapenzi ulikufa mwaka 2016 baada ya mrembo huyo kujihakikishia kwamba mpenzi wake alichepuka na mbaya zaidi amefanya hivyo na ndugu yake wa damu, kisha na rafiki yake.
 
Sadio Mane

Sadio Mane ameweza kuyafanya maisha yake binafsi kutofahamika kwa wengi. Ni jambo gumu kutambua kama staa huyo wa Liverpool ana mchumba au hana. Siku zote amekuwa akihudhuria matukio mbalimbali akiwa peke yake na familia yake tu ndicho kitu ambacho amekuwa akikizungumza mara kwa mara.
 
Kylian Mbappe

Macho ya wengi yameelekezwa kwa kinda wa Ufaransa, Kylian Mbappe, baada ya mchezaji huyo kuisaidia timu hiyo kuichapa Argentina kwenye fainali hizi za Kombe la Dunia na kutinga robo fainali kabla ya kuichapa Uruguay kutinga nusu fainali.
 
Kiwango chake kimeripotiwa kumvutia Miss Ufaransa 2017, Alicia Aylies, ambaye alikuwapo uwanjani kumshangilia. Lakini, ukweli ni kwamba Mbappe muda wote amekuwa bize kutengeneza maisha yake ya soka ili yawe na mafanikio zaidi akiyapa kisogo masuala ya kuwa na mchumba kwa sababu hayapo kwenye mipango yake kwa sasa zaidi ya kuwanyoosha tu mabeki uwanjani.
 
Back
Top Bottom