Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ufaransa imefuzu fainali ya Kombe la Dunia, baada ya kuifunga Ubelgiji bao 1-0, katika mchezo mkali uliochezwa kwenye Uwanja wa St Petersburg nchini Russia.

Ufaransa imepania kurudia rekodi ya mwaka 1998 ilipotwaa ubingwa wa Kombe la Dunia katika fainali zilizochezwa nchini humo huku kocha wa sasa wa timu hiyo, Didier Deschamps akiwa nahodha.
 
Bao pekee lililofungwa na beki wa kati wa Ufaransa anayecheza klabu ya Barcelona Samuel Umtiti, liliipeleka Ufaransa fainali. Timu hiyo inasubiri mshindi wa mchezo wa kesho baina ya England na Croatia kucheza fainali Jumapili wiki hii mjini Moscow.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…