Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

CROATIA...
1280px-Casco_viejo_de_Dubrovnik%2C_Croacia%2C_2014-04-14%2C_DD_02.JPG
 
Dakika 45 za mwanzo Ubelgiji ilicheza soka maridadi huku nahodha wake Edin Hazard anayecheza klabu ya Chelsea akicheza kwa kiwango bora ingawa mashuti yake mengi yalitua mikononi mwa kipa mkongwe Hugo Lloris.
 
Licha ya Ubelgiji kutawala sehemu kubwa ya mchezo, lakini ilishindwa kupenya ukuta uliokuwa chini ya beki wa Real Madrid Raphael Verane na Umtiti.

Ufaransa ilifuzu nusu fainali baada ya kuilaza Uruguay mabao 2-0 wakati Ubelgiji ilipenya kwa ushindi wa mabao 2-1 ilipovaana na Brazil.
 
Baada ya kupatikana kwa mbabe kati ya Ubelgiji na Ufaransa, uso wa dunia utageuka kutoka St. Petersburg, kuelekea mji mkuu wa Moscow. Safari ya masaa nane na dakika 48, takribani kilomita 714.1 itahusika kuwatoa mashabiki 81,000 kutoka St. Petersburg, kwenda kuujaza uwanja wa taifa.
 
Majira ya saa tatu ya usiku wa leo, Uwanja wa Luzhniki utafurika. Runinga zote kote duniani, zitakuwa zinaonesha kitu kimoja, mechi ya kukata na shoka ya nusu fainali ya pili ya Kombe la Dunia 2018, kati ya Croatia na England. Hatumwi mtu dukani wallahi!
 
Ni hivi, rekodi zinaonesha kuwa, mara ya mwisho, England ilipofuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii mikubwa duniani, Croatia ndio kwanza ilikuwa inahangaika kutafuta uhuru wake, kutoka umoja wa Yugoslavia, achilia mbali kufikiria kuwa na timu ya taifa.
 
Namaanisha, katika soka, Croatia ni watoto wadogo sana kwa England. England wakiongozwa na Malkia wao, Bibi Elizabeth wa tatu, usiku wa leo wanakutana Croatia na Rais wao, Mwanamama Kolinda Grabar-Kitarović, katika dimba la Luzhniki, wakiwa na shauku kubwa inayosumbua nyoyo zao.
 
Wababe hawa wanaingia Luzhniki wakiwa na shauku ya kuweka rekodi mbili tofauti. Wakati Croatia wao wataingia katika mchezo huu wakiwa na shauku ya kutinga fainali kwa mara ya kwanza katika historia ya soka lao, England watakuwa na nia ya kutoa gundu la miaka 52 ya kulikosa kombe hili. Patachimbika aisee!
 
Turudi nyuma kidogo. Wakati Kocha wa Croatia anachukua mikoba ya ukocha katika timu ya taifa ya Croatia (2017), alikuwa na kibarua cha kupata mfumo mzuri ambao ungemruhusu kuwatumia moja ya viungo bora duniani kwa sasa bila tabu. Nawazungumzia Luca Modric (Real Madrid) na Ivan Rakitic (Barcelona).
 
Back
Top Bottom