Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

446736779_56997.jpg
 
Kwa tuliokwenda kusoma na tukaamua kubobea kwenye maeneo machache hasa eneo la "BRANDING" tunapata shida sana.

Hivi ni kweli kuwa hii ndege mpya inayotarajiwa kuwa imeandikwa "HAPA KAZI TU"?Kama ni kweli nadhani tujadiliane kama imekidhi vigezo vyote vya "Marketing strategy" pamoja na "How to establish brand".

1.Nadhani hii ndege imelenga sana soko la kimataifa na siyo soko la ndani,sijui kwa nini kama hii ni kweli,wanamkakati wameamua kutumia "Local slogan" kama tunazozishuhudia kwenye mabasi ya ndani ambayo ndiyo tumezoe kuona yameandikwa,MTAJIJU,BABA YAKO ANAYO?,NA BADO,WEWE UNANISEMA MIMI NAINGIZA n.k.

2.Slogan tunaambiwa ni vizuri ikatengeneza "Sense of ownership" ama "We feeling" pamoja na Positive Emotion appeling kwa watu.

3.Kwa nini tusingetuma Slogan ambayo ingeenda kuitangaza Tanzania na vivutio vyake?Watanzania tunafahamu kama"The most amazing place in the world"ipo Tanzania?,tunafahama,"Fresh water" duniani baada ya ile ya Urusi inapatikana Tanzania?Kwa nini tusije na "Slogan"ambayo ndege hii ikikaa pale Frunkfurt,ama Amsterdam,ama Washington,ama Quatar,itasaidia kuuuambia Ulimwengu kuwa,"The most amazing place"ipo Tanzania?Nawaza kwa unyenyekevu.

Hebu Tanzania walichokifanya Rwanda,wamekwenda London na kuandika kwenye jezi za Arsenal,"VISIT RWANDA"unaiona mantiki.

4.Kikubwa nilichokiona kwenye"Slogan" hii naona ni suala zuri na lina hitaji mjadala pia tumetumia Kiswahili,tumekiuza Kiswahili,hili laweza kuwa jema lakini bado tujadiliane .

Wanamkakati wa "Slogan" hii wanadhani inaviashiria vya "Sense of ownership" kwa watanzania wote? je itawafanya watanzania wote bila kujali tofauti zao kusema hii yetu,tuilinde,tuifie,tuichangie?

Kwa nia njema kabisa,tuitazame upya hii Slogan kimkakati kibiashara,kama ni kweli imeandikwa ili iwe na "Sense of Ownership".pamoja na "International marketing eye".Karibu Tujadiliane.kwa Unyenyekevu na nia njema kabisa na uweledi wa hali ya juu.

Ipo siku itakuja ndege nyingine na wanamkakati wetu wataiandika "WATAPATA TABU SANA"na tutaona sawa tu.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom