Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Star umpendaye ana trend kwa story gani mtandaoni?. Muigizaji wa kike Genevieve Nnaji ame trend kwenye mitandao ya kijamii nchini Nigeria kwa kumaliza ujenzi wa estate yenye nyumba nyingi za kupangisha. Genevieve aliwahi ku-post picha moja miaka miwili iliyopita ikiwa ni sehemu ya ujenzi wa estate hiyo. Sasa hivi imekamilika na anataraji kuwa mama mwenye nyumba nyingi za thamani na wapangaji wakimlipa kodi kubwa kila mwezi. . . . Huyo ni muigizaji wa Nigeria,
 
Ronaldo kulipwa billioni 1.6 kwa wiki - Millioni 10 kwa saa! . Baada ya jana kutangazwa kujiunga na klabu ya Juventus FC ya Turin Italia - sasa imeripotiwa kwamba Cristiano Ronaldo ataingiza jumla ya billioni 324 kwa miaka 4 atakayoitumikia Juventus kutokana malipo ya mshahara tu bila kuweka marupurupu mengineyo. Mpira unalipa wewe!! ; Huu hapa ndio mchanganuo ya malipo ya Ronaldo akiwa Juventus kwa fedha za madafu! . Bilioni 324 kwa miaka 4. Bilioni 81 kwa mwaka. Bilioni 6.75 kwa mwezi. Bilioni 1.6875 kwa wiki. Milioni 241 kwa siku. Milioni 10 kwa saa. Laki 167,000 kwa dakika. 2,800 kwa sekunde.
 
RAIS Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, amewasili nchini kimyakimya akiwa na familia yake. Hii ni mara ya pili kwa Obama kuja nchini, ambapo mara ya kwanza ilikuwa Julai 2013, wakati kiongozi huyo akiwa bado madarakani. Ziara yake hiyo ya kikazi ilikuwa ni sehemu ya kukamilisha ratiba yake ya mwisho ya ziara barani Afrika wakati akiwa Rais. Tofauti na ziara yake ya awali ambapo alikuja na ndege ya Air Force One akiwa na msafara unaolindwa na kila aina ya teknolojia, safari hii alikuja na familia yake lengo likielezwa kuwa ni kwa ajili ya kupumzika. Chanzo cha uhakika kililiambia MTANZANIA kuwa Obama alitua nchini kimyakimya ambapo aliwasilia Jumapili ya Julai 8, mwaka huu ana kushukia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kufanya mazungumzo na kiongozi mmoja mwandamizi wa Serikali katika eneo maalumu ambalo lilitengwa mjini Moshi. Baada ya mazungumzo na kiongozi huyo wa Serikali yaliyodumu kwa takribani dakika 40, Obama alirejea KIA akiwa kwenye gari maalumu na kupanda ndege ndogo maalumu na kwenda kupumzika Mbuga ya Serengeti. “Alipanda ndege ndogo akaenda Serengeti ambapo amefikia Singita Grumeti,” kilisema chanzo chetu. Pamoja na hali hiyo inaelezwa kuwa Rais huyo Mstaafu wa Marekani, atakuwa hapa nchini kwa mapumziko ya wiki moja pamoja na familia yake. Akiwa ndani ya Mbuga ya Serengeti atajionea utajiri mkubwa wa maliasili uliopo nchini pamoja na vivutio vyake ikiwamo wanyama. Katika ziara yake ya mwaka 2013, Obama aliisifu Tanzania na kusema ni kama nyumbani kwake, kutokana na historia yake. Alisema uhusiano uliopo kati yake na Tanzania, umewafanya baadhi ya wanafamilia wake kuwa na uhusiano wa kuitembelea Tanzania kwa shughuli mbalimbali. Katika mkutano wake na wanahabari uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa na mwenyeji wake wakati huo Rais Mstaafu Jakaka Kikwete, Obama alisema anajisikia fahari kuitembelea Tanzania, kwani ni moja ya nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambayo anatoka baba yake. Alisema Marekani na Tanzania, zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu ambao uliwekwa na marais waliotangalia wa nchi hizo, akiwemo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa 35 wa Marekani.
 
Klabu ya Arsenal imekamilisha kumsajili kiungo Mfaransa Matteo Guendouzi,19,kutoka Lorient kwa pauni milioni 8. Kiungo huyo anakuwa ni usajili watano wa Arsenal katika majira haya ya kiangazi. Kocha wa sasa wa Arsenal ni Unai Emery, na si Arsene Wenger.
 
Gari ya kubebea Wagonjwa (Ambulance) ya Hospitali ya Wilaya ya Tarime imekamatwa ikiwa imebeba Kilo 800 za Dawa za Kulevya aina ya Mirungi. RPC wa Mara amethibitisha kukamatwa kwa gari hilo na watu wawili, gari ilikuwa inatoka Mwanza kwenda Tarime.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…