Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ndani ya saa 12, mchezaji wa JKU, Feisal Salum Abdalah “FEI TOTO” amesaini mkataba wa miaka mitatu asubuhi Singida United, ghafla Yanga imepindua meza kwa kumsainisha mchezaji huyo mkataba wa miaka mitatu jioni hii katika ofisi zao zilizopo mitaa ya Jangwani.
 
Mapema leo asubuhi Singida United ilitoa picha cha Fei Toto akiwa anasaini mkataba wa miaka miaka mitatu na klabu hiyo pamoja na kuvalishwa jezi.

Hata hivyo leo mchana mabingwa wa kihistoria, Yanga nao walitoa video za picha za Fei Toto akiwa na viongozi wa JKU pamoja na wale wa Yanga.
 
Yanga ni kama wameipiga bao Singida United kwani walianza kutoa picha zikimuonyesha mchezaji huyo anasaini akiwa na Mkurugenzi wa Singida United, Festus Sanga.

Kupitia kwa Meneja wa mchezaji huyo, Mohammed Kombo, alisema Singida hawakufata utaratibu na badala yake walikiuka taratibu zinazohitajika katika usajili.
 
Feisal mpaka jioni saa kumi na nusu alikuwa bado mchezaji wa JKU, lakini kuanzia sasa ni mchezaji halali wa Yanga baada ya wao kumalizana na sisi," alisema Kombo.

Naye Feisal alisema yeye ni mali ya Yanga na anatarajia kufanya mazuri akiwa na kikosi hiko.
 
Feisal mpaka jioni saa kumi na nusu alikuwa bado mchezaji wa JKU, lakini kuanzia sasa ni mchezaji halali wa Yanga baada ya wao kumalizana na sisi," alisema Kombo.

Naye Feisal alisema yeye ni mali ya Yanga na anatarajia kufanya mazuri akiwa na kikosi hiko.
 
AKIWA na umri wa miaka 19, Kylian Mbappe, amekuwa matata kweli kweli uwanjani na hakika hakamatiki kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 zinazoendelea kule Russia.

Kikosi chake cha Ufaransa kimeshatinga fainali ya michuano hiyo huku Mbappe akipewa nafasi ya kuibuka kidedea kwenye Tuzo ya Mchezaji Bora Kijana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…