Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20180711-WA0008.jpg
 
Lakini, wanakwambia hivi, kuna wachezaji wanne hao walikuwa moto zaidi walipokuwa na umri kama wa Mbappe na hao jamaa wanafanya mambo kiasi cha kumfanya Mfaransa huyo aonekane kuwa ni wa kawaida tu, yaana hana maajabu!
 
4.Eden Hazard

Mbappe na Eden Hazard wote walianza kucheza soka la kulipwa wakiwa na umri wa miaka 16. Hazard alianza kucheza mwaka 2007, alipokuwa na umri huo.

Mbappe yeye alianza kucheza soka la kulipwa mwaka 2015 alipokuwa na umri huo. Wakiwa na umri wa miaka 17, wote Hazard na Mbappe walikuwa wachezaji wenye umri mdogo zaidi kufunga kwenye vikosi vya kwanza vya timu zao.
 
Mbappe alikuwa Monaco na Hazard alikuwa Lille. Lakini, kuna tofauti baina ya washambuliaji hao. Hazard akiwa na umri wa miaka 17 tu akaanza kuichezea timu ya taifa na hiyo ilikuwa mwaka 2008, wakati Mbappe alianza kuichezea timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 18 na hiyo ilikuwa mwaka 2017.
 
3.Neymar Jr.

Neymar alianza kubamba kwenye vyombo vya habari akiwa na umri mdogo sana. Santos FC ilimpa ofa ya mkataba mwaka 2003, kipindi hicho akiwa na umri wa miaka 11 na kumwingiza kwenye akademi yao. Akiwa na umri wa miaka 14, Neymar alisafiri hadi Hispania kwenda kwenye timu ya watoto ya Real Madrid, lakini dili halikuwa zuri. Akiwa na umri wa miaka 15, Neymar alianza kuwa na msaada kwa familia yake akiinunua nyumba kwa pesa alizovuna kwenye soka.
 
Alikuwa akilipwa pesa ya Kibrazili 10,000 kwa mwezi na alipofika miaka 16 alikuwa akilipwa 125,000 kwa mwezi. Alifunga bao kwenye mechi yake ya kwanza baada ya dakika 28 tu za kuwa uwanjani na hiy ilikuwa mwaka 2010, kipindi hicho alikuwa na umri wa miaka 18.
 
Back
Top Bottom