Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wafanyakazi wa Kampuni ya utengenezaji magari ya Fiat Chrysler nchini Italia wamekerwa na kitendo cha mmiliki mwenye hisa nyingi ndani ya kampuni hiyo kuamua kutoa Eiro 112 milioni sawa na Pauni 99.2 milioni kumsajili Cristiano Ronaldo kwenda Juventus.
 
Wamekerwa na uamuzi wa kumsajili Ronaldo kutoka Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne ulioigharimu klabu hiyo Pauni 99 milioni ambazo inaaminika zinatoka mfuko mwa bilionea huyo, ambazo bila shaka zitakua sehemu ya mtaji wa Kampuni hiyo ya magari ambayo imeanza kuyumba kwa karibu miaka miwili sasa.
 
Mtaalamu wa fedha kwenye soka, Rob Wilson, kutoka Sheffield Hallam University, amesema hana wasiwasi kuwa Juventus itarudha fedha za kumnunua Ronaldo ndani ya mda mfupi na anaamini klabu hiyo itakusanya fedha nyingi kutokana na kumsajili mshambuliaji huyo nyota duniani.
 
Biashara inaonyesha kuwa Juventus wamelamba bingo kwa usajili huu, watavuna kiasi kikubwa cha fedha lakini pia uwanjani Ronaldo atawasaidia sana hasa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya nadhani watapata faida mara dufu,” alisema Wilson.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…