Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

LUCA MODRIC.
Kiungo wa Real Madrid Luca MODRIC ambaye juzi alitangazwa mchezaji bora wa kombe la Dunia, amepokea ofa kadhaa za timu za ligi kuu England, ipielo. Chalsea, Liverpool na timu yake ya zamani ya Tottenham zinaumana kumrudisha Modric England. Modric mwenyewe hajaamua hatma yake ingawa Madrid bado wanamuhitaji:- Mashirika ya habari
 
LIVERPOOL na Atletico Madrid zinasuguana zikimuwania beki kisiki wa Croatia na Besiktas, Domangoj Vida aliyetamba kwenye kombe la dunia akipigania taifa lake. Beki huyo mpenda ubabe na anayetumia nguvu inadaiwa thanani yake ni pauni 31 milioni. Anaweza kuondoka kwenye dirisha hili kubwa la usajiri ikiwa bei hiyo itafikiwa
 
Steven N' Zonzi
Barcelona imeingia kwenye mbio za kumfukuzia kiungo wa Sevilla Steven N'Zonzi ambaye pia anafukuziwa kimya kimya na kocha Arsenal Unai Emery.hapo kabla Barcelona iliweka kipaumbele chake kwa kiungo wa PSG, Adrien Rabiot ambaye pia ni mfaransa, lakini imeachana na wazo hilo na kuelekeza silaha zake zote kwa N'Zonzi ambaye hapo juzi ametwaa medali ya dhahabu kwa kutwaa kombe la Dunia akiwa na kikosi cha Ufaransa
 
MARIO MANDZUKIC
Borussia Dortmund ya Bundesliga ina mpango wa kumtwaa mshambulizi wa Juventus Turin Mario Mandzukic ambaye anaweza kuondoka timu hiyo baada ya ujio wa Ronaldo, mchezaji huyo ambaye ana mkataba na timu hiyo wa mpaka mwaka 2020 alikuwa mmoja wa wachezaji walioing'arisha Croatia kwenye kombe la Dunia huko Urusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…