Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Maelfu ya wananchi walijitokeza kuwalaki wachezaji hao, huku wakipeperusha bendera za nchi hiyo kuonyesha furaha yao.

Mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo za kuwahamasisha wakiwataka wasikate tamaa kwa hatua kubwa kwa kucheza fainali.
 
Shabiki mmoja alisema wanajivunia na kikosi chao kufikia hatua kubwa, huku wakisema wanawahesabia kama mashujaa katika kipindi chote cha maisha yao.

Aliongeza kuwa tangu nchi hiyo ipate uhuru haijawahi kutokea kile walichokifanya wachezaji hao mashujaa, huku akisistiza wataendelea kuwa na mapenzi na timu hiyo ambayo imeibuka shujaa.
 
KYLIAN Mbappe amedai kwamba anataka kubaki kwenye chama la Paris Saint-Germain.

Lakini, staa wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand amemwambia Jose Mourinho kufanya kweli kwenda kumsajili mshambuliaji huyo wa Ufaransa ili aje Old Trafford haraka.
 
Ishu ya Mbappe ipo hivi, PSG alicheza kwa mkopo msimu uliopita na wababe hao wa Ufaransa wanapaswa kuilipa AS Monaco Pauni 166 mwaka huu ili kumbeba jumlajumla. Shida inakuja sehemu moja tu, PSG wanachunguzwa kwa sasa kuhusu matumizi yao ya pesa kwenye usajili na huenda wakabaswa wasimbebe jumla mchezaji huyo kutokana na kubanwa na sheria ya usawa kwenye usajili hasa baada ya kutumia Euro 222 milioni kumsajili Neymar msimu uliopita.
 
Man United sasa imeshtukia dili na kupanga kuweka mezani mzigo wa Euro 300 milioni kumnasa kinda huyo bora kabisa kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika juzi Jumapili huko Russia, ambako alifunga mabao manne. Hata hivyo, Man United watakabiliwa na upinzani mkali kwenye mpango wao huo kutokana na staa huyo kuwapo kwenye orodha ya wakali wanaosakwa na Real Madrid ili kwenda kuziba pengo la Cristiano Ronaldo huko Bernabeu. Kwa mujibu wa Don Balon, Man United ina uhakika kwamba Euro 300 milioni za kumsajili Mbappe zitapatikana tu, kwa sababu kuna mpango wa kumpiga bei Paul Pogba kwa Euro 150 milioni.
 
Ujio wa Mbappe kwenye kikosi cha Man United kama utafanikiwa basi utaifanya timu hiyo kuwa na kikosi matata kabisa, lakini utakuja kumtikisa Alexis Sanchez, ambaye atahitaji kuonyesha ubora mkubwa msimu ujao ili kuendana na mshahara anaolipwa kila wiki kwa huduma yake anayotoa huko Old Trafford. Man United wamepanga kumpa Mbappe ofa ya mshahara wa Euro 45 milioni kwa mwaka kabla ya makato ya kodi.
 
Mashabiki wa soka jijini Paris, Ufaransa walimefurika kuipokea timu yao jana Jumatatu baada ya kutwaa Kombe la Dunia kwa kuishindilia Croatia mabao 4-2 juzi Jumapili.

Mashabiki hao waliojitokeza jijini Paris walitinga nguo zilizokuwa na rangi ya bluu, nyekundu na nyeupe kuashiria rangi za bendera za Taifa hilo.
 
Wananchi walisikika wakiimba nyimbo za kuwapongeza wachezaji pamoja na benchi la ufundi waliokuwa kwenye gari maalumu ya wazi huku ikikatiza mitaa ya jijini Paris.

Gari hilo liliolokuwa likisindikizwa na ving’ora vya polisi lilizingira pia na maaskari walikuwa wakikimbia kwa mwendo wa wastani kwa ajili ya kuimaisha usalama wa wachezaji hao.
 
Masaa mawili baada ya timu hiyo kutua kutoka nchini Russia, kikosi cha timu hiyo kilipokewa na Rais wa nchi hiyo, Emmanuel Macron.

Rais huyo akiwa ameambatana na mke wake walliwakaribisha wachezaji hao kwenye viwanja vya Ikulu vya nchi hiyo.

Ndege maalumu ziliwalaki kwa heshima wachezaji hao, huku zikiacha michirizi ya yenye alama za bendera ya Ufaransa.
 
JOSE Mourinho bana anapotaka lake, amekuwa mjanjamjanja sana. Si unafahamu kwa sasa anaifukuzia huduma ya winga wa Inter Milan na Croatia, Ivan Perisic, basi anachojaribu kufanya ni kumtetea na kumsifu staa huyo kila siku ili kumshawishi achague kwenda kujiunga na kikosi chake cha Manchester United huko Old Trafford.
 
Mourinho amtetea winga huyo kwamba hakushika mpira makusudi kwenye fainali ya Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Ufaransa juzi Jumapili na kumfanya mwamuzi Nester Pitana kuamuru ipigwe penalti baada ya kwenda kuangalizia picha za marudio ya tukio hilo kupitia VAR. Kauli ya Mourinho anaonekana kuguswa kabisa na kile kilichotokea dhidi ya mchezaji huyo anayemtaka aende kwenye timu yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…