Naunga mkopo mfumo huu wa VAR, lakini si kwa kile kilichofanyika kwenye fainali. Niliunga mkono mfumo huo nikiamini kwamba ungeondoa yale makosa makubwa kwenye soka, lakini si kutumika kwa ajili ya kutoa penalti tu na mengi haitumiki," alisema Mourinho.
Imeonekana wazi kuna makosa. Hivi Perisic angerukaje juu na mkono wake ukiwa chini. Angewezaje kufanya hicho wanachosema wakati hatua chache mbele yake kulikuwa na mchezaji wa Ufaransa? Fainali si mechi ya kawaida, kufanya uamuzi ule wa VAR ulileta athari kubwa kwenye mechi.”
Kwenye dirisha lililopita, Perisic alifikia makubaliano binafsi kujiunga na Man United, lakini wababe hao wa Old Trafford walishindwa kukubaliana na Inter Milan kwenye ada ya uhamisho. Sasa Mourinho amepania kuinasa huduma yake hasa baada ya kutamba kwenye Kombe la Dunia 2018.