Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Keshasahau kuwa mwenyewe juzi juzi tu hapa alikaribia kwenda huko huko?
mtz16.jpg
 
Ben R. Mtobwa

Hata nipewe week kumuelezea huyu mwandishi haitoshi

watanzania bado tuna kiu sana ya kupata waandishi bora kama hawa

ndio maana kila siku tunamuimba Shaaban Robert na wenzake wachache

nani atatukata hii kiu???
Waandishi wapo wengi tu. Shida ni wasomaji wa kazi zao. Vitu hivi huenda pamoja.
 
wasomaji wapo mkuu

mbona Shaaban na Ben walisomwa sana na watanzania hawa hawa?

Ipo shida mahali
Tafiti zimeshaonyesha kuwa usomaji wa vitabu umeporomoka sana kwa Tanzania. Riwaya pendwa za kipelelezi za akina Musiba, Katalambula, Mtobwa na waandishi wengineo zilivutia wasomaji wengi katika miaka ya 80 na kipindi hicho kinatambuliwa leo kuwa kipindi bora kabisa katika fasihi ya Kiswahili. Leo hii mpaka ubahatishe kitabu chako kiingizwe katika mitaala ya shule. Watu hawaoni sababu ya kuingia gharama kuchapisha kitabu wakati mauzo yake ni hasara tupu.

Kuna makala mengi ya kitaaluma kuhusu jambo hili na kwa nini leo vitabu vingi vinatoka Kenya.
 
Back
Top Bottom