Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Paris Saint-Germain ndiyo klabu iliyofunga mabao mengi zaidi 13 katika Kombe la Dunia Russia wakifuatiwa na Tottenham Hotspur.

Chipukizi Kylian Mbappe ameng’ara katika mashindano hayo akifunga mabao manne, akifutiwa na washambuliaji wenzake wa PSG, Edinson Cavani (matatu) na Neymar (mawili) wengi waliofunga bao mmoja ni Thiago Silva, Angel Di Maria, Thomas Meunier na Grzegorz Krychowiak.
 
Shukrani kwa Harry Kane alifunga mabao sita na kunyakuwa kiatu cha adhabu na kuiongoza Spurs kufunga mabao 12, wengi waliofunga ni Heung Min Son (mawili) huku Christian Eriksen, Dele Alli, Kieran Trippier na Jan Vertonghen kila moja alifunga bao mmoja
 
Timu tatu za LaLiga zilikamilisha idadi ya timu tano zilizofunga mabao mengi, Barcelona ilipata mabao 11, huku beki wake Yerry Mina akiongoza kwa mabao matatu, huku Luis Suarez na Philippe Coutinho kila moja amefunga mabao mawili.
 
NI mwendo wa nipe nikupe. Baada ya kuizuia Arsenal, Petr Cech katika dirisha la majira ya joto mwaka 2015, Chelsea sasa imepewa fursa ya kumrudisha kipa huyo katika milingoti yao wakati huu kipa, Thibaut Courtois akitazamiwa kusaini Real Madrid.

Cech alitua Arsenal kwa ruhusa ya tajiri Roman Abramovich akisaini mkataba wa miaka mitano kwa dau la pauni 10 milioni licha ya kuichezea klabu hiyo ya Stamford Bridge kwa miaka 11 lakini sasa anaweza kurudi nyumbani.
 
Kocha mpya wa Arsenal, Unai Emery ametoa ruhusa kwa kipa huyo wa kimataifa wa Czech kuondoka Emirates baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya kipa wa kimataifa wa Ujerumani, Bernd Leno kutoka Bayer Leverkusen katika dirisha hili.
 
Chelsea ipo katika msako wa kipa na pia inavutika na mpango wa kumnasa kipa wa Leicester City, Kasper Schmeichel ambaye aling’ara katika michuano ya kombe la dunia na kikosi cha Denmark. Lakini pia wamekuwa wakimfukuzia kipa wa AC Milan na timu ya taifa ya Italia, Gianluigi Donnarumma.
 
Cech anakaribishwa tena Stamford Bridge kutokana na mtu aliyechukua maamuzi ya kumuondoa, kocha wa zamani, Jose Mourinho kutimuliwa klabuni hapo na sasa ni kocha wa Manchester United. Lakini kocha Unai analazimika kuachana na kipa mmoja kati ya Cech au David Ospina kwa ajili ya kuwa na makipa wawili wa kimataifa.
 
Kipa huyo wa Cezch aliyetwaa ubingwa wa England mara nne pamoja na ubingwa wa Ulaya mara moja akiwa na Chelsea ana uhusiano mzuri na mashabiki wa Chelsea pamoja na mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia, kitu ambacho kinaweza kusaidia arudi Stamford Bridge kiulaini.
 
Klabu zote mbili zimeingia kwa kasi katika dirisha hili la uhamisho licha ya Chelsea kuanza kwa kusuasua mwanzoni mwa dirisha hili kutokana na sintofahamu iliyokuwa inamkabili kocha wao aliyetimuliwa, Antonio Conte.
 
Wakati Arsenal ikiwa imewachukua, Stephan Lichtsteiner, Sokratis Papastathapoulos, Matteo Guendouzi, Lucas Torreira na Leno, Chelsea mpaka sasa imefanikiwa kumpora kiungo wa kimataifa wa Italia mzaliwa wa Brazil, Jorginho ambaye alikuwa anaelekea Manchester City.
 
Wakati Arsenal wakidaiwa kumfukuzia kwa karibu kiungo wa Sevilla, Steven N’Zonzi ambaye alikuwepo katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa kombe la dunia nchini Russia Jumapili iliyopita, Chelsea imekuwa ikiwalenga wachezaji kibao.
 
Kocha Maurizio Sarri ana matumaini kwamba Chelsea itakamilisha uhamisho wa kiungo wa mahiri wa CSKA Moscow, Aleksandr Golovin aliyenga’ara katika michuano ya kombe la dunia nchini Russia kwa dau la pauni 22 milioni. Kwa kufanya hivyo, Chelsea itakuwa imeipiga bao Monaco ambayo pia inamuwinda staa huyo.
 
Sarri pia amekuwa akihusishwa na mlinzi wa Napoli ya italia, Kalidou Koulibaly pamoja na staa wa Juventus, Daniele Rugani huku akitazamiwa kuachana na walinzi wake mahiri wa kati, Gary Cahill na David Luiz ambao nafasi zao zimekuwa zikisuasua tangu msimu uliopita chini ya kocha, Conte.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…