MANCHESTER United imeamua kuwapima imani mashabiki wake maana bei wanayouza jezi zake mpya watakazotumia msimu ujao wa 2018/19 inahitaji uvumilivu.
Ni hivi, kwa shabiki atakayehitaji seti nzima, kwa maana ya jezi ya juu na bukta yake basi atalazimika kulipa Pauni 192, ambazo ukichenji kwa pesa ya Kitanzania hiyo ni Sh574,937 na kwa pesa ya Kikenya ni Sh25,263. Si kupimana imani huku?