Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

imeshawaweka kikosini wakali Naby Keita, Xherdan Shaqiri na kipa wa Kibrazili, Alisson Becker.
Fabinho alisema kwamba amekuwa akitumia muda wake kumshawishi mchezaji mwenzake wa zamani wa Monaco, Mbappe kuhamia Liverpool kwa sababu wamekuwa wakizungumza na alimpongeza kwa uhamisho huo.
 
Kylian alitumia meseji kunipongeza kwa kuhamia Liverpool," alisema Fabinho na kuongeza.
"Bado sijapata nafasi ya kumpongeza kwa kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia. Walichofanya Ufaransa kiliwa safi na alichofanya Mbappe kwa miaka miwili ya karibuni babkubwa. Anahitaji pongezi kubwa na nitafanya hivyo kumpongeza. Ameshasema kwamba msimu ujao atabaki PSG, lakini taratibu
 
KWENYE udhia penyeza rupia. Mwezi Januari Liverpool ilitatua tatizo la beki kwa kuvunja rekodi ya uhamisho ya dunia ilipomnunua Virgil van Dijik. Safari hii imetatua tatizo la kipa kwa kuvunja rekodi ya uhamisho wa makipa.
 
Hatimaye Liverpool imefanikiwa kumnasa kipa namba moja wa Timu ya Taifa ya Brazil na AS Roma, Alisson kwa kiasi cha Pauni 67 milioni ambacho kinavunja rekodi ya uhamisho wa makipa duniani. Ni jeuri kubwa ya pesa.
 
Staa huyo wa Brazil amelazimika kukatisha likizo yake katika Visiwa vya Sardinia kwa ajili ya kwenda Liverpool juzi Jumanne na jana alitazamiwa kupimwa afya Anfield kabla ya kusaini mkataba wa miaka sita na wababe hao waliokuwa na tatizo la kipa.
 
Mkurugenzi wa Ufundi wa Liverpool, Michael Edwards alifikia makubaliano na mkurugenzi mwenzake wa ufundi wa Roma, Monchi ambapo sasa Liverpool italipa kiasi cha Pauni 58.5 milioni mbele kisha kumalizia Pauni 9 milioni baadaye.
 
Awali ofa ya Pauni 62 milioni ya Liverpool ilikataliwa na Roma lakini Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp hakuona umuhimu wa kupoteza muda na kuanza kusumbuana na Chelsea na Real Madri ambazo pia zilikuwa zinamtaka kipa huyo. Ikamalizia ilichotaka Roma.
 
Awali ofa ya Pauni 62 milioni ya Liverpool ilikataliwa na Roma lakini Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp hakuona umuhimu wa kupoteza muda na kuanza kusumbuana na Chelsea na Real Madri ambazo pia zilikuwa zinamtaka kipa huyo. Ikamalizia ilichotaka Roma.
 
Uhamisho wa Alisson kwa sasa unakuwa mara mbili ya rekodi ya awali ya uhamisho wa makipa ambayo iliwekwa na kipa wa Manchester City, Ederson aliyehamia klabuni hapo kwa dau la Pauni 35 milioni miezi 12 iliyopita. Ederson ni kipa wa pili katika kikosi cha Brazil.
 
Hakutarajiwi kuwa na matatizo yoyote katika mazungumzo ya maslahi binafsi baina ya kipa huyo na Liverpool na klabu hiyo imedhamiria kumtangaza Alisson kama usajili wake wa nne katika dirisha hili kabla haijaondoka kwenda Marekani leo Ijumaa kwa maandalizi ya msimu mpya.
 
Hata hivyo, kipa huyo hataungana na wenzake katika ziara hiyo ambayo itaiona Liverpool ikicheza dhidi ya Manchester United, Manchester City na Borussia Dortmund kwa vile ana wiki nzima ya kuendelea na likizo yake baada ya Brazil kufika robo fainali katika Kombe la Dunia.
 
Kuwasili kwa kipa huyo kunamaanisha huenda ukawa mwisho wa kipa, Loris Karius ambaye alikuwa anaaminiwa na Kocha Klopp lakini akafanya makosa katika pambano la fainali za Ulaya dhidi ya Real Madrid Mei mwaka huu na hata katika mechi za maandalizi ya msimu mpya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…