Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

E32DB350-4599-4DAD-A562-339B175E8B92.jpeg
 
Methali 31:10-31

10 Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha marijani.
11 Moyo wa mumewe humwamini, Wala hatakosa kupata mapato.
12 Humtendea mema wala si mabaya, Siku zote za maisha yake.
13 Hutafuta sufu na kitani; Hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
14 Afanana na merikebu za biashara; Huleta chakula chake kutoka mbali.
16 Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
17 Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi; Hutia mikono yake nguvu.
18 Huona kama bidhaa yake ina faida; Taa yake haizimiki usiku.
19 Hutia mikono yake katika kusokota; Na mikono yake huishika pia.
20 Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake.
21 Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake; Maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
22 Hujifanyia mazulia ya urembo; Mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
23 Mume wake hujulikana malangoni; Aketipo pamoja na wazee wa nchi.
24 Hufanya nguo za kitani na kuziuza; Huwapa wafanya biashara mishipi.
25 Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao.
26 Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake.
27 Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu.
28 Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema,
29 Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote.
30 Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
31 Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
 
MANCHESTER City wameshusha mitambo miwili hadi sasa, Riyad Mahrez na Philippe Sandler na wote hao imewanasa kwa Euro 68 milioni.

Manchester United ishanasa mitambo mitatu hadi sasa, Fred, Diogo Dalott na Lee Grant, ambao wote wamegharimu Euro 82.7 milioni.
 
Liverpool ndio wamefanya balaa, wameleta mitambo minne, Naby Keita, Fabinho, Xherdan Shaqiri kwa Euro 199.7 milioni. Chelsea wanakwenda mdogomdogo, mtambo walionasa hadi sasa ni Jorginho, aliyewagharimu Euro 57 milioni.
 
Tottenham Hotspur wao bado wanasuasua, hawajaleta mtambo mpya, bado wanaamini katika ile ya zamani. Hata hivyo, baadhi ya wachezaji hao wapya bado hawajiunga na timu zao kwa sababu wengine walikuwa na timu zao za taifa kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia, hivyo watakuwa na siku nyingi zaidi za kupumzika.
 
Kocha Unai Emery huko kwenye kikosi cha Arsenal, majaribio ya mwisho kabisa ya kikosi chake atayafanyia kwenye mechi dhidi ya Sevilla itakayopigwa Agosti 4 na baada ya hapo, msimu utakuwa unaanza, ambapo atakuwa na shughuli ya kuwakabili Man City. Pep Guardiola, ubora wa mitambo yake atatesti kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich, itakayopigwa Julai 28 na baada ya hapo, atakuwa amepata majibu atoke vipi kwa msimu ujao.
 
Jose Mourinho, ambaye kwa sasa yupo na kikosi chake cha Man United huko Marekani na wachezaji wengi wakiwa makinda, anaamini hadi Agosti 5 atakuwa na nyota wake wote, ambapo atatesti mitambo yake kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich huko mjini Munich, Ujerumani na baada ya hapo kazi itahamia kwenye Ligi Kuu England. Mauricio Pochettino na Spurs yake atatesti mitambo kwenye mechi dhidi ya Girona huko Hispania, Agosti 4
 
wakati Jurgen Klopp na Liverpool yake atakuwa amefahamu ubora wa mitambo yake kabla ya kuanza kwa msimu mpya wakati atakapoijaribu kwenye mechi dhidi ya Torino, Agosti 7 uwanjani Anfield. Hivyo, ndivyo makocha wa Top Six kwenye Ligi Kuu England watakavyotesti mitambo yao kabla ya kuanza rasmi kwa mchakamchaka wa msimu mpya.
 
MAMBO ya Unai Emery huko Arsenal si mchezo unaambiwa.

Supastaa Mesut Ozil ameamua kukatisha mapumziko yake na kurudi Arsenal fasta baada ya wachezaji wenzake kumwaambia utamu wa mazoezi ya Emery, ambaye kwa sasa ametua kwenye kikosi hicho kuchukua mikoba ya Arsene Wenger, aliyeng'atuka mwishoni mwa msimu uliopita.
 
Back
Top Bottom