PANYA alikuwa na msongo wa mawazo kwa sababu aliogopa sana paka. Akatokea mchawi mmoja mkubwa sana; kwa haruma, akamgeuza kuwa paka. Akiwa paka, akaanza kuogopa mbwa, hivyo, yule mchawi akamgeuza kuwa mbwa. Akiwa mbwa akawa anaogopa sana chui. Yule mchawi, kwa huruma zaidi, akamgeuza tena na kuwa chui. Haikuchukua muda, akaanza kuogopa wawindaji. Mwishowe, yule mchawi alichoka, akaamua kumrudisha kuwa paka na kumwambia: "Hakuna ninachowezafanya kikakusaidia, kwa sababu umeshindwa kutambua ukuaji wako. Aheri tu urudi ulivyokuwa mwanzo!"
Usipotambua ukuaji wako na kuzitumia nguvu (fursa) zako, basi siku moja, hofu unazoziendekeza zitakurudisha nyuma.