Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

NAMNA YA KUTENGENEZA JUISI YA UKWAJU.
Nunua ukwaju wako, ukwaju unapatikana kwa wingi sana masokoni na kwenye supermarketsAndaa maji kwenye dishi na uoshe kidogo tuu baada ya kuuosha chukua ukwaju wako weka kwenye sufuria yenye maji ya saizi na injika jikoni uache uchemke kwa dakika 10/15 ili uuwe vijidudu Ipua ukwaju wako jikoni na uache kwa muda upoe andaa maji yako masafi na chujio ili uweze kuchuja juice yako kwa uangalifu zaidi ili upate juice yenyewe Weka sukari kwa kiasi unachopendelea pia ili kupunguza ukali unaweza ukaweka hiliki au vanila ili kupata taste weka juice yako kwenye fridge ili ipoe tayari kwa kunywa.
 
FAIDA YA JUISI YA UKWAJU.
Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini 'antioxidants' ambavyo huzuia Saratani (cancer)Chanzo cha Vitamini B na C vile vile "carotentes"Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumboHuulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooniHusaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwaHusaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)Husaidia kurahisisha choo (laxative)Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyoHusaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye vidondaHusaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)
 
Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!

Unatakiwa ujaribu kuweka
ukwaju karibu katika kila mlo
wako kwa kila siku kwasababu
ukwaju una faida nyingi kiafya
ambazo hakika zitakufanya uwe
na afya njema au kukuimarisha
afya yako kiujumla
 
Watu waishio bara la Asia,
Carribian na America ya kusini
wanajua kuwa kula ukwaju
maana yake ni Afya Njema.

Ukwaju unaoliwaa katika maeneo
haya maeneo hayo una faida
nyingi kwa watu wanaoula.
 
Kwa hiyo siku nyingine unapoenda
kufanya manunuzi ya vyakula
hakikisha unanunua na ukwaju.
Ukwaju ni zao la rangi ya kahawia
ambalo limefungwa na kasha
gumu. Ndani ya kasha hilo kuna
vifundo vilaini ambavyo ndani
yake kuna mbegu nyeusi.
 
Vifundo
hivi ndiyo ambavyo watu
wanakula ili kupata virutubisho na
faida za kiafya za ukwaju. Ukwaju
una ladha faluni ya uchachu
ukiwa bado mchanga, lakini kadiri
unavyozidi kukomaa unakuwa na
ladha tamu. Ingawa ukwaju
unakuwa na utamu kadiri
unavyokuwa na kukomaa,
kiujumla ukwaju ni mchachu.
 
Katika nchi kama Jamaica, Mexico,
Aruba na India, ukwaju
unachanganjwa na sukari na
kuuzwa kama pipi katika mitaa na
madukani. Kula ukwajua au
bidhaa zitokanazo na ukwaju
kuna faida sana. Ukwaju umejaa
Vitamini, fiber, potassium,
magnesium na virutubisho
vingine muhimu kwa afya njema.
 
Lakini kati ya faida zingine nyingi
za virutubisho na kiafya za
ukwaju, kuna kadhaa ambazo ni
za muhimu zaidi, na ni kama
zifuatazo:

1. Ukwaju chanzo kizuri sana cha
antioxidants ambazo zinasaidia
kupigana na saratani. Ukwaju
una carotenes, Vitamini C,
flavanoids na vitamin B zote.
 
Aisee ukwaju umenisaidia sana kwenye hali yangu hii, kuna time mambo yalikuwa si shwari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…