Hii maana yake nini?Jumla ya kata 22 kati ya 77 ambazo utafanyika uchaguzi wa marudio tayari chama tawala CCM kimepita bila kupingwa baada ya wagombea wa vyama vya upinzani kuwekewa pingamizi ikiwemo madai ya kudaiwa kukosea kujaza fomu.
Tangu mwaka 1994(ulifanyika uchaguzi mdogo),Tanzania ilipofanya uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi haijawahi tokea poromoko kubwa kama hili la wagombea kufyekwa hivi.
Kama katika ngazi ya udiwani hali ipo hivi,naona dalili za Mwakani kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa na vijiji wagombea wengi kujikuta wanakosa haki ya kugombea kwa sababu kama
hizi zilizoelezwa kwenye hili linaloendelea la uchaguzi mdogo.
Jambo linalofikirisha zaidi,kwa nini wanaodaiwa kutojua utaratibu wa kujaza fomu wanatoka upinzani?vyama vya upinzani nchini Tanzania havina mfumo wa kuwaelimisha wagombea wao namna ya kujaza fomu bila kukosea?
Kwa hali hii,mwakani kwenye uchaguzi wa serikali za mtaa na vijiji,kuna uwezekano wakafyekwa wengi na tukashuhudia labda asilimia 50 ya vijiji na mitaa watu wakapiga kura za ndiyo na hapana.
Nadhani kuna haja,Tume ya uchaguzi,kituo cha demokrasia Tanzania,vyombo vya habari ,vyama vya siasa vyenyewe,asasi za kiraia zinazojikita kwenye kutoa elimu ya Uraia kulichukua hili kwa uzito wake kwa ustawi wa siasa za Tanzania.