Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG_20180724_063706_326.jpg
 
Badilika

Wala msifuatishe namna ya Dunia hii, Bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu .

1.Anza kujifikiria wewe mwenyewe kwanza ni tabia gani unayoitaka na ipi huitaki, Unao uwezo mkubwa ndani yako, ila hujajua kuutumia.

Hapo Mwanzo Mungu aliziumba Mbingu Na Nchi, Nayo Nchi ilikuwa Ukiwa, Utupu Na Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji.Roho ya Mungu ikatulia juu ya maji, Mungu akasema iwe Nuru , Ikawa Nuru.
 
2.Rudia Rudia Tabia unayoitaka na itakuwa ya kwako. kama vile Yoshua alivyoambiwa , kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku. Yoshua 1:8

Tabia nzuri ni ngumu kuitengeneza lakini ni rahisi kuiishi. Tabia mbaya ni rahisi kuitengeneza lakini ni ngumu sana kuiishi.
 
3.Ukiamka Asubuhi kila siku sema asante Mungu, Kwa wema wako, Asante kwa Upendo, Asante kwa mafanikio, Asante kwa vitu ambavyo tayari ninavyo.

Shukuruni kwa Kila Jambo maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo. 1Wathesalonike 5:18

Siri ya mafanikio yako inategemea Agenda yako, utakavyokuwa kesho fanya leo. uwe na lengo la siku, wiki, mwezi, mwaka, miaka.
 
4.Ukitaka kufanikiwa kuwa na tabia njema au kitu kingine chochote , utahitaji NIDHAMU na Kukipenda kitu unachokitaka. Unatakiwa ufanye kila siku kila siku. sio leo unafanya , kesho hufanyi, hutaweza kufanikiwa. sema haya maneno kila siku kila wakati . Muombe Mungu akupe Upendo, Furaha, Amani, Utu wema, Uvumilivu, Fadhili, Upole , Uaminifu na Nidhamu.

Vitatokea kwako.
 
Back
Top Bottom