Usipopangilia masaa yako vizuri , hutaweza kupunguza uzito ulionao. Dawa kubwa ya kupunguza uzito wako ni kujua kutumia muda wako vizuri. Usiwe mtu wa kukaa muda mrefu bila ya kufanya kitu chochote. Anza leo kupunguza muda wa kukaa kijiweni kuongea habari za mpira, acha kukaa barazani kuongea umbea, acha kukaa kwenye Tv muda mrefu kutazama movies. Badala yake soma vitabu, nenda kwenye seminar mbalimbali, tafuta makala nzuri jifunze kupigana na ujinga. Acha kupigana na umaskini. Hutaweza kusikia njaa hovyo hovyo kama utafanya hivi vitu .