Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unaweza kubadilisha mfumo wa maisha , ukaanza kutumia muda vizuri, unakuwa mwaminifu kazini kwenye ndoa , biashara. unakuwa makini ni vitu gani vinaingia akilini mwako. unalisha nini roho yako, unalisha nini mwili wako. Unasikiliza vitu gani, una mitazamo gani.
 
Ukijitahidi katika kutafuta kiini cha tatizo ni rahisi kupona badala ya kutumia dawa ambazo zina madhara makubwa.

Nguvu ya uongo ipo ndani ya mtu . Badili mtazamo wako, badili tabia yako, Acha kulalamika, kulaumu watu, kujilaumu mwenyewe, kusononeka, kujihukumu. shughulikia akili yako, roho yako na mawazo yako pamoja na mwili wako.
 
Kuwa mtu wa shukrani. Mkumbuke Mungu, Msifu Mungu, Mshukuru Mungu . Anza kampeni ya kumtafuta Mungu kwa bidii kama una tatizo la kiafya.

Utaanza kuona unapona magonjwa, umaskini katika kila hali .kutumia dawa bila kutubu ni sawa na kwenda kwa mganga wa kienyeji. TUBU kwanza
 
Bila kusamehewa dhambi hutaweza kupona ugonjwa ulionao. Anza na Mungu maliza na Mungu. Kumbuka kuwa Dactari anatibu lakini Mungu Anaponya. Neno la Mungu linaponya.

Elimu inatibu Hofu , lakini Imani inaponya Hofu.
 
Zaidi na zaidi tunajifunza kila siku kuhusu kupunguza uzito, sio tu katika mazoezi na kupunguza calories.

Tunapozingitia mwili wa mwanadamu kwa ujumla na kuelewa umuhimu wake, tunaweza kuamua kwamba tunachokiona kwenye kipimo ni namba ndogo kuliko kinachoendelea ndani ya miili yetu.
 
Hii ni kwa habari zote nzuri na mbaya. Kwa msaada mwingine , tunapohangaikia uzito wetu, hatutakiwi kuona ugumu ; kutunza uzito sio tu katika nidhamu na kujidhibiti. kwa upande mwingine, ina maana kwamba ili kufikia uzito wa kufurahisha na kubaki nao huo uzito , inabidi kufanya kazi ya kutosha ili kuiponya mifumo wa miili yetu kuanzia ndani.
 
Kwa kushughulikia matumbo yetu, hormoni zetu, kiasi cha sukari. Kuacha dhambi. kujifunza kutumia muda vizuri kuliko kupoteza muda kutazama TV, instagram, Facebook na mitandao mingine. Badala yake tuwe na utaratibu wa kujisomea kwa bidii, Hasa vitabu vya Hekima kama Biblia, Kurani, na vingine. Vitabu vya wenye hekima. Kutafuta maarifa .
 
Kazi ya pesa ni kukokoa muda sio za kutumia kwenye Chips Kuku,Pombe, Nyama choma, Ugali mkubwa, Nyama choma nyingi, vyakula vilivyotunzwa kwenye makopo. Tumia pesa katika kutafuta taarifa sahihi, kununua CD za magunzo mazuri. vitabu vya wenye Hekima, sikiliza Video zenye msukumo .

Anza kupunguza uzito wako leo, hapa nakuambia kwa nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…