Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5.Vincent Kompany – Man City

Umri wa sasa wa Vincent Kompany ni miaka 32 na kichwani kwake hakuna nywele kabisa. Kwa miaka kadhaa, Kompany amekuwa hana chaguo la kubadilisha mitindo yake ya nywele zaidi ya kunyoa upara tu.

Wachezaji wengine wamekuwa na kawaida ya kubadili mitindo mbalimbali ya nywele, lakini kwa Kompany mambo ni tofauti, hana nywele katikati, hivyo ni mwendo wa kipara tu.
 
4.Miranda – Inter Milan

Kumwona Mbrazili mwenye uaraza hilo ni jambo la kawaida kutokana na Waamerika Kusini kufahamika zaidi kwa jambo hilo. Beki wa kati wa Inter Milan, Miranda ni miongoni mwao. Mchezaji huyo umri wake ni miaka 33, lakini tayari amekuwa na uharaza.

Miranda hafahamiki sana kwa uhamisho wake wa kukaba kwenye beki, bali kwa kufunga mabao muhimu na upara wake kwenye mechi muhimu.
 
3.Fabian Delph – Man City

Fabian Delph amekuwa akifahamika kwa staili yake moja tu ya nywele tangu alipoanza soka la kulipwa 2006. Beki huyo wa kushoto wa Manchester City na uaraza, akiwa na umri wa miaka 28 tu. Kutokana na kukosa nywele kwenye sehemu ya utosi, Delph amejikuta akiwa mwenye staili moja tu ya nywele zake ni kunyoa upara tu, hana chaguo jingine.
 
2.Arjen Robben – Bayern Munich

Ni jambo gumu kuamini Arjen Robben kuna wakati kichwa chake chote kilikuwa na nywele.

Lakini winga huyo wa Bayern Munich alianza kupoteza nywele zake akiwa kwenye umri mdogo sana. Alianza kupata uharaza akiwa na umri wa miaka 24 na hadi sasa anaonekana kama mzee vile.

Umri wake ni miaka 34, lakini ukikutana naye hapo, uaraza unamfanya aonekane babu.
 
1.Lucas Moura – Tottenham

Lucas Moura ndiyo kwanza ana umri wa miaka 25, lakini ile paap umekutana naye, utadhani umekutana na mzee wa miaka 70.

Uharaza umemfanya aonekane mzee na jambo baya, ameanza kupoteza nywele akiwa mdogo, na umri mdogo sana. Nywele zake zilipukutika wakati akiwa kwenye kikosi cha Paris Saint Germain alichodumu nacho kwa miaka sita. Jambo hilo limemfanya kuwa na staili moja tu ya nywele zake, kunyoa upara tangu akiwa na umri wa miaka 21.
 
KOCHA Unai Emery unaambiwa mbinu zake mpya zitamfanya fundi wa mpira Mesut Ozil kurudi kwenye ubora wake.

Kocha huyo mpya wa Arsenal, Emery amerithi shughuli pevu kutoka kwa mtangulizi wake Arsene Wenger kuhakikisha anapata namna nzuri ya kumtumia mchezaji wao huyo, waliyemsajili kwa Pauni 42.5 milioni kutoka Real Madrid.
 
Kazi ya kumrudisha kwenye ubora wake Ozil inazidi kuwa ngumu baada ya kufanya hovyo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 zilizofanyika Russia huku lawama nyingi zikielekezwa kwake kwa kitendo cha Ujerumani kukomea hatua ya makundi kwenye fainali hizo
 
Kwenye fainali hizo za Russia, Ozil alicheza kwa dakika 180 na sasa ameungana na kikosi cha Arsenal kilichokwenda Singapore kwa ajili ya mechi za kirafiki.

Emery alisema: “Tupo hapa kumsaidia kila mchezaji. Kwa upande wangu mchezaji mmoja ni sawa na wachezaji 25. Kwetu sisi, Ozil ni mchezaji muhimu sana, hivyo tutamsaidia kuhakikisha anakuwa vizuri, anakuwa bora kwetu.
 
Mwaka jana ulikuwa mgumu kwa kila mtu, si kwa Ozil peke yake. Walimaliza nafasi ya sita kwenye ligi na hiyo si nafasi aliyoitaka. Kutokana na hilo, tunakuja na mbinu mpya za kumrudisha kwenye ubora wake. Nataka kufanya naye kazi na kumsaidia kurudi kwenye ubora wake ambao utatufanya tuwe vizuri kama timu.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…