HAKIKA HUYU MWANAMKE SI WA NCHI HII, KUNA KITU HAPA!
__________________________________
Mke na mume waligombana, mume akamwambia mkewe abebe kila anachoona anakipenda na aondoke aende zake kwao. Mke bila hiyana akachukua mito miwili tu vingine vyote akaviacha pale pale.
Wakati anajiaandaa kutoka akapiga simu ili gari lije limchukue lakini kabla hajatoka akamwambia mumewe,"kwakua ulikuja kunichukia nyumbani kwetu kipindi unanichumbia basi na leo nakuomba unirudishe mume wangu kipenzi ".
Mume akakubali ,walivyofika nyumbani kwa mwanamke (ukweni) mke akamwambia mumewe"samahani naomba uingie chumbani kwangu mara moja kabla hujaondoka ninashida kidogo/kuna kitu nataka kukwambia "Mume akakubali na akaingia kisha mke akamfungia mlango kwa nje dhen yeye akatoka .
Baada ya muda jamaa akaona kimya ,akaamua ampigie simu mama mkwe wake ili amweleze kile alichofanyiwa na mkewe.
Mama mkwe naye akampigia simu binti yake ili amuulize kama kuna tatizo, binti akajibu "ndiyo lipo "akaelezea kama ilivyokua kuhusu ugomvi na mwisho akamalizia kwakusema "mume wangu kaniambia nibebe vitu ninavyovipenda ndo nikamchukua na yeye nimekuja nae kwasababu nampenda sana mume wangu nisingiweza kumuacha nyumbani pekeake .
Ni upendo wa ajabu sana. Mwanamke popote ulipo kunywa twist nitalipia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]