SOMA HII HADI MWISHO:
Mwanajeshi alikuwa vitani akipigana vita dhidi ya
adui. Upande wake wenzake wote waliuawa
isipokuwa yeye peke yake.
Mwanajeshi baada ya kuona amezidiwa na
anaweza kuuawa wakati wowote, aliamua
kukimbia kwa kasi kuelekea asikokujua. Alifika
latika mwamba mkubwa wa mawe ambako
alishindwa kupanda ili kuwakwepa wale adui
zake.
Hivyo akaanza kuomba kwa Mungu amuepushie
na hilo janga, kwani anajua kama angekamatwa
angeuawa vibaya sana. "Mwenyezi Mungu niokoe
na hiki kifo kilicho mbele yangu, na nitaishi
nikikuabudu wewe"
Wakati akiendelea kushangaa shangaa pale,
akaona kuna mapango kadhaa chini ya ule
mwamba wa mawe, hivyo akaamua kuingia ndani
ya pango mojawapo. Akiwa ndani akasikia adui
zake wakimtafuta pango moja baada ya jingine
"atakua ameingia humu, hebu chungulieni"-
alisikia wakiambizana na kama pango lilikuwa
giza walililipua na bomu ili yoyote aliyemo ndani
afie humo humo.
Mwanajeshi aliingiwa na wasiwasi mno maana
alijua kwamba wakifika katika pango ambalo
yumo, hata wakimchungulia wasipomkuta
watalipua tu bomu na yeye atafia humo.
Hivyo akazidi kumuomba Mungu, "Oh Mungu
wangu, niokoe na hiki kifo kibaya"- wakati
akiendelea kuomba akaona buibui akitokea mbele
ya lile pango kwenye ule mlango, buibui akaanza
kujenga utando (web) wake.
Askari akamuuliza Mungu, "Badala ya kuliziba
pango na mawe makubwa, umetuma buibui ndio
ajenge utando?? Itawezaje kuniokoa mimi? Baada
ya kuona hilo askari akapoteza matumaini ya
kupona na akalala tu pale kusubiri kulipuliwa.
Baada ya maadui kufika katika pango alilopo,
Mwanajeshi mmoja akataka kurusha bomu ndani,
ila kamanda wake akamkaripia..."wewe
mpumbavu, huoni huo utando wa bui bui hapo
kwenye mlango wa pango? Unataka kumaliza tu
bomu zetu chache zilizobaki.
Yule askari aliyetaka kulipua akamuuliza
kamanda wake, "unamaanisha nini kamanda?"
Kamanda akajibu, "ninamaanisha kwamba kama
huyu mpumbavu mmoja aliyebaki angekimbilia
humu basi angevunja huo utando wa bui bui,
sasa buibui alivyojitanda hapo na huo utando
wake huyo mtu angeingiaje bila kuuvunja? kifupi
hamna mtu humo, twendeni mbele tutamkamatia
huko huko, hivyo wakaondoka na kuendelea
kulipua mapango yaliyofuata.
Askari akawa ameokoka na kifo.....akiwa ndani
ya pango akainama na kumwambia Mungu
"Nisamehe Mungu wangu kwa kudharau njia
zako, asante kwa kuokoa maisha yangu"
Mpendwa, katika siku hizi za mwisho wa dunia
unaweza ukawa katika matatizo makubwa, lakini
kamwe usichoke kumuomba Mungu. Mungu
anaweza kukujibu kwa namna yake yoyote ile
inaweza ikawa ndogo tofauti na wewe
ulivyofikiria. Ila usisahau kwamba utando wa
buibui uliojengwa na Mungu ni imara zaidi ya
ukuta wa matofali uliojengwa na binadamu.
Share ujumbe huu na
Mungu akafanye njia pasipo njia kuwa na njia
katika maisha yako